Waha katika ramani
Waha
ni
kabila
kubwa
[1]
[2]
la
watu
wa
Tanzania
wanaoishi katika
Mkoa wa Kigoma
hadi mpakani kwa
Burundi
.
Lugha
yao ni
Kiha
, jamii ya
Kirundi
,
Kinyarwanda
na
Kihangaza
katika
kundi
la
lugha za Kibantu
.
Katika kipindi cha kuhamahama kwa ajili ya kutafuta
masilahi
kama vile
chakula
na kukimbia
vita
, wazazi wa kabila hilo, baada ya kufika kando ya
ziwa Tanganyika
na maeneo yote yanayolizunguka Ziwa Tanganyika waliweza kukaa na kuanzisha shughuli mbalimbali kama vile
kilimo
,
uvuvi
,
ufugaji
na
uwindaji
.
Waha walipoanza kuyazoea mazingira, walijigamba na kujidai kwa makundi ya kikoo kuwa yana nguvu, kila mmoja kwa nafasi yake. Kila
ukoo
ulijigamba kwa kutumia majina ya
wanyama
,
wadudu
,
ndege
,
milima
n.k.
Waha wanagawanyika kati ya Wahambwe (Waha wa Kibondo), Wayungu (Waha wa Kakonko), Washingo (Waha wa Heru Bushingo) na Wanyaheru (Waha wa Heru Juu) mbali na
Wamanyema
(ambao si Waha, wana asili ya
Kongo
). Hao wote, pamoja na kuwa wavuvi na wachuuzi, ni wakulima wa mazao mbalimbali kama vile mahindi, maharage, mtama, karanga, viazi, mihogo n.k.
Waha pia ni wavuvi wa samaki katika ziwa Tanganyika,
mto Malagarasi
,
Mto Rwiche
,
Mto Mkoza
, na mito mingine midogomidogo kama vile, Nyajijima, Mresi, Kazingu, n.k.
Waha ni
wafugaji
wa
ng'ombe
,
mbuzi
,
kuku
,
bata
,
nguruwe
,
sungura
,
mbwa
,
paka
, n.k.
Biashara
zao ni mazao wanayoyalima, samaki, na
bidhaa
nyingine za kawaida.
Usafiri
wao wa asili ulikuwa wa
miguu
yao wenyewe, ambapo kuna
imani
ilikuwepo pia ya kusadikika kuwa walitumia
ungo
kusafiria kama
ndege
yao ya asili.
Utamaduni
wao, yaani ma
vazi
yao ilikuwa ni magome ya
miti
yaliyojulikana kama
impuzu
, na
nyumba
zao za
msonge
,
udongo
na miti, kulingana na sehemu mbalimbali, maana kuna sehemu zenye
joto
kama vile
bondeni
, na sehemu zenye
baridi
kama vile
nyanda za juu
. Kwa sasa wanatumia zaidi kitenge.
Historia ya jina
Historia ya Waha ilianzia katika
kijiji
kiitwacho Buha kilichopo Heru: hapo ndipo Waha walipofikia baada ya kutoka maeneo ya
Burundi
,
Rwanda
na
Kongo
.
Inafahamika kuwa Waha ni moja ya makabila kutoka Wabantu wa mashariki. Wabantu hao walipata kufika maeneo hayo hata kabla ya miaka ya 600 yaani kabla ya Wamanyema. Wamanyema na Waha ndio wenyeji wa Kigoma. Uenyeji huu tunaouzungumza ni miaka ya zamani sana: hata kabla ya kuanza kwa ukoloni hawa watu tayari walikuwa wakiishi pamoja na walikuwa wakipendana na kuthaminiana. Kuna vitu Waha waliwafundisha Wamanyema na pia kuna vitu Wamanyema waliwafundisha Waha na wote hawa waliipigania Tanganyika kutoka mikononi mwa serikali ya kikoloni. Hata mradi wa kuligawa
bara
la Afrika kati ya nchi kadhaa za
Ulaya
ulikuwa bado kabisa Wamanyema na Waha walikuwa wakiishi pamoja.
Ifahamike kuwa asilimia kubwa ya makabila mengi yaliyopo hapa Afrika yalipata majina kulingana na wageni walivyoelewa au walivyoona. Kuna makabila yaliyopata majina kutokana na namna wanavyopigana, yapo makabila yaliyopata majina namna wanavyopiga makelele na wengine walipewa majina kulingana na
lugha
yao au matamshi yao. Kwa upande wa kabila la Waha, ambao wanapatikana katika mkoa wa Kigoma, ukweli ni kwamba kabila hili ni miongoni mwa makabila ambayo yana historia kubwa sana tangu walipofika katika ardhi hiyo na pia ni kabila lenye umaarufu mkubwa nchini.
Kipindi watu hawa wanafika maeneo ya
Afrika Mashariki
hawakujulikana kama kabila la Ha na hawakuja wakiwa kundi moja. Bali walikuja kwa mtindo wa koo na kila
ukoo
ulikuwa na jina lake.
Koo zilizokuwa hapo zilipata kumiliki ardhi. cha msingi ni kwamba watu hao walifanikiwa kuitwa majina ya maeneo waliyokaa kutokana na
mazingira
yake. Kwa mfano kuna ukoo uliokaa sehemu zenye
udongo
(Bayungu) walijiita Wayungu na wale waliokaa sehemu za mwinuko (Heru) walijiita Wanyaheru. Lakini mpaka kufikia miaka ya 1800, koo hizo ziliungana na kuishi sehemu na kutawaliwa na
chifu
mmoja. Ndipo watu hao walipoanza kupata jina moja lililowatambulisha kwa wageni.
Sasa kwa nini watu hao waliitwa Waha? Hii ndiyo mitazamo iliyosimulia asili ya neno Waha au Ha.
1. Wapo waliodai kuwa asili ya neno Waha au Ha ni pale wageni walipofika katika ardhi ya Kigoma na kuwauliza watu hao kuwa “ninyi ni wakina nani” na ndipo watu hao walipojibu “tur; Abhaha” wakimaanisha "sisi ni wazaliwa wa hapa hapa". Hapo wageni hao walikariri kuwa Waha kwa kuchukua neno “ha”,,, Kiuhalisia Waha na Wamanyema ni watu wamoja: tangu enzi na enzi walipendana na kuthaminiana.
2. Wapo wanaodai kuwa wageni walipokuja na kukuta ufalme wa Buha umekua na ulikuwa na watu wengi, walimuuliza
mfalme
wao kuwa “hawa ni wakina nani”, na ndipo mfalme wa Buha alipojibu kuwa, “N’abhaha” akimaanisha kuwa “hawa ni wenyeji wa hapahapa” na hapo wageni hao walipata neno “Ha” na walipoandika waliaandika hivyo.
Maelezo hayo yalitolewa na watu waliokuwa wamekutwa katika ardhi ya Buha. Kwa upande mwingine, historia inafafanua kuwa,
Watusi
walikuwa watawala wa kabila la Waha na kuna mahusiano makubwa sana kati ya Watusi na Waha. Hivyo hata neno Waha bado lilionekana kuhusiana na Watusi.
Kwa Watusi neno Abaha lina maana ya mtu yeyote “anaowapa ardhi” na kwa Watusi aliyekuwa akitoa ardhi alifahamika kwa jina la Mtoke. Na mteko alikuwa akitoa ardhi kwa Watusi, walifahamika kwa jina moja la Uwaha.
Waliolima shamba moja na Mteko walijiita “Abhaha”, hata kuna baadhi ya Watusi hujiita “Waha” na ndiyo maana hata walivyotawala walijiita hivyo.
Tanbihi
Marejeo
- J.H. Scherer,
Marriage and Bride-Wealth in the Highlands of Buha (Tanganyika)
. Diss. Utrecht University, 1965.
Viungo vya nje