Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Valletta
(pia:
La Valetta
, kwa
Kimalta
:
il-belt
"mji") ni
mji mkuu
wa
Malta
wenye wakazi 7,100.
Mji
ulijengwa kama mji-boma kwenye ncha ya
rasi
ndogo inayozungukwa na
maji
ya
bahari
pande tatu.
Valletta limepokea
jina
lake kwa
heshima
ya
Jean de la Valette
aliyekuwa mkuu wa
Wanamisalaba
wa
chama cha hospitali ya Mt. Yohane wa Yerusalemu
. Valette aliamuru kujengwa kwa mji huu baada ya uvamizi wa
Waturuki
waliojaribu kuteka Malta
mwaka
1565
. Waturuki hawakufaulu wakafukuzwa na Valette aliona haja ya kuwa na mji imara kabisa kama hao watataka kurudi. Hivyo mji mpya ulijengwa kuanzia mwaka
1566
kwenye ncha ya rasi yenye
bandari
asilia bora.
Mnamo mwaka
1700
Valetta ilikuwa mji wenye
ukuta
imara kushinda miji yote.
Mji una
majengo
mengi ya
kihistoria
hata ukaingizwa katika orodha ya
UNESCO
ya
urithi wa dunia
.
Idadi
ya wakazi imepungua kwa sababu watu wengi walikwenda kujenga
mashambani
.
|
Makala hii kuhusu maeneo ya
Ulaya
bado ni
mbegu
.
Je unajua kitu kuhusu
Valletta
kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|