Maghofu ya
Zeila
, Somalia iliyokuwa bandari kuu ya Adal.
Usultani wa Adal
(
Kisomali
: Adaal,
Kige'ez
: ???
?Ad?l
,
Kiarabu
: ???; c.
1415
-
1555
) ulikuwa
dola
la
Kiislamu
miaka
1415
hadi
1577
katika maeneo ya
Ethiopia
ya
mashariki
,
Jibuti
na
Somaliland
ya leo. Katika kipindi cha juu cha uwezo wake, Adal ilitawala sehemu kubwa za maeneo ya Ethiopia na
Somalia
.
[1]
Adal ilifuata kipindi cha
Usultani wa Ifat
. Baada ya
usultani
huo wa Kiislamu kushindwa kabisa na
ufalme
wa Ethiopia mnamo
mwaka
1415, sehemu ya
familia
ya
watawala
chini ya
Haqq ad-Din II
walihamia maeneo ya
Harar
na
Hargeisa
walipoanzisha Adal.
Mji mkuu
wa kwanza ulikuwa
Dakkar
uliofuatwa baadaye na Harar.
Wakazi wa sehemu hizo na pia
askari
wa
jeshi
lake walikuwa hasa
Wasomali
na
Waafar
.
[2]
Viongozi wake, hasa Ahmad ibn Ibrihim al-Ghazi au
Ahmad Gran
, walitazamwa kama
Wasomali
.
[3]
Tangu mwaka
1288
, Adal ilikuwa eneo la Waislamu. Eneo la mtawala wa
Kikristo
wa Ethiopia aliyeitwa wa
nasaba ya Solomoni
. Muda mfupi, baadae eneo hili lilipiganiwa na kuwa chini na Ethiopia.
Negus Negesti
Amda Seyonna
kampeni zake za mwaka 1332. Katika kipindi hiki, Mfalme wa
Shewa
Na Mfalme wa
Ifat
waliokuwa wakiongoza misafara ya kibiashara na bandari katika mwambao wa , pamoja na mfalme wa
Zeila
pia walitekwa.Baadae Adal ilikuja kuongozwa na Ifat, lakini baadea ilikuja kuwa huru baada ya mapigano yake dhidi ya Amde Seyon, lakini baadae tena, walijisalimisha baada ya Mfalme wao kufariki na kutekwa kwa mji mkuu wao wao
Talag
Na huo ndio ukawa mwisho Jamal ad-Din wa Ifat na ufalme wake.
[4]
Katika mwaka kati ya 1403 au 1415, Waethiopia walivamia tena Ifat ambayo ndio tu ilikua imetoka katika mapigano, na kuweza kuwapiga maadui zao chini ya Mfalme wao.
Sa'ad ad-Din II
. Sa'ad ad-Din alifukuzwa kutoka katika utawala wao na ufalme wa Ethiopia, hii ikiwa ni mwaka 1403 au
Yeshaq I
in 1415) na baadae kuvamia eneo la
Zeila
na kumuua. Matokeo yake Familia za matajiri waliondoka nchini humona kukimbilia nchini Yemen kuepuka kukamatwa na kuuwawa. Walipokuja kurejea, walikuta tayari ufalme umebadilishwa kutoka jina la Mfalme wa Ifat na kuwa Mfalme Adal hii ikionesha kuwa, Ifat ilikuwa sehemu ya Adal.
Katika miaka ya katika ya 1520 Imam
Ahmad ibn Ibrihim al-Ghazi
Aliivamia Adal na kutangaza rasmi vita takatifu dhidi ya wakristu wa Ethiopia.ambao kwa wakati huo walikuwa chini ta utawala wa
Lebna Dengel
. Wakiwa wanapewa zana za kupigania kutoka katika Ufalme wa Ottoman,. Ahmad aliweza kuwapiga waethiopia katika vita vya
Battle of Shimbra Kure
mwaka 1529, na kuweza kuchukua mali zote kutoka Ethiopia, kama vile maeneo ya mwinuko, japokuwa waethiopia waliendelea kukataa kuachia maeneo hayo. Mwaka 1541, Ureno ambayo ilikuwa wakihitaji baadhi ya maeneo katika Bahari ya Hindi, walituma msaada wa askari kwa Waethiopia. Na kwa kujibu suala hilo, Adal nao wakapokea askari 900 kutoka katika ufalme wa
Ottomans
Imam Ahmad aliweza kufanikiwa katika mapigano dhidi ya Waethiopians, wakati akiendelea na kampeni katika Autumn mwaka 1542. Aliweza kumuua kiongozi wa kijeshi wa Ureno,
Cristovao da Gama
mwezi Agosti mwaka huo huo. Hatahivyo wapiganaji wa Kireno walikataa kujisalimisha kutokana na kifo cha Adal katika vita vya
Battle of Wayna Daga
, karibu na ziwa Tana mwezi Februari mwaka 1543, ambapo Ahmad aliuwawa katika vita hivyo. Kutokana na hali hiyo, Waethiopia waliweza kuchuakua uwanda wa juu ulioinuka walioupateza baada ya kushindwa katika vita dhidi ya Adal. Mwaka 1577, mji mkuu wa Adal na uliamishiwa kutoka
Zeila
na kwenda
Harar
n hii ilifuatia kuanguka kwa utawala wa Adal.
- ↑
Travis J. Owens: Beleaguered Muslim fortresses and Ethiopian imperial expansion from the 13th to the 16th century, June 2008 Monterey, CA 93943-5000 (M.A. Thesis), [
https://apps.dtic.mil/dtic/tr/fulltext/u2/a483490.pdf
online hapa]
- ↑
Herausgegeben von Uhlig, Siegbert,
Encyclopaedia Aethiopica
. Wiesbaden:Harrassowitz Verlag, 2003, pp.71
- ↑
ibid
, pp. 155
- ↑
ibid
, pp.71
|
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Usultani wa Adal
kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|