Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Usiku
ni kipindi cha
siku
kilichopo kati ya
machweo
na
macheo
na hasahasa kipindi cha
giza
kinachotokea baada ya machweo ambapo
mwanga
wa
jua
hauonekani tena
angani
hadi muda mfupi kabla ya macheo yaani kabla ya jua kuonekana juu ya upeo wa anga.
Kinyume chake ni
mchana
.
Kutokana na kupoteapotea kwa
nuru
ya jua,
nyota
zinaonekana usiku (pasipo ma
wingu
).
Watu wengi pamoja na
wanyama
wengi hulala usiku, lakini kuna wanyama wengine wanaofanya
shughuli
zao usiku kama vile
bundi
,
popo
na
wadudu
wengi.
Nyakati za mwanzo na mwisho wa usiku hutofautiana kati ya
mahali
na mahali
duniani
.
Mstari
unaofikiwa na mwanga wa jua unatembea juu ya
uso wa dunia
kutokana na
mzunguko
wa dunia kwenye
mhimili
wake.
Mwendo
huu ndio
sababu
ya kugawiwa kwa uso wa dunia katika
kanda muda
.
Karibu na
ikweta
muda wa usiku ni ma
saa
12 sawa na muda wa mchana, lakini penginepo duniani, kadiri palipo mbali na ikweta kuelekea
kaskazini
au
kusini
, muda wa usiku hubadilika kila siku.
Usiku mrefu kabisa hutokea kwenye
ncha za dunia
ambako wala jua wala
utusitusi
havionekani angani kwa muda wa karibu miezi 3.
Katika tamaduni za
binadamu
usiku mara nyingi una maana mbaya kutokana na ma
tatizo
ya kutoona vema na
hofu
ya vitu visivyoonekana katika kipindi hicho.
Wikamusi
ya Kiswahili ina maelezo na tafsiri ya maana ya neno: