Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Uchaguzi wa Rais wa Marekani, mwaka wa 1968
ulikuwa wa 46 katika historia ya Marekani. Ukafanywa Jumanne tarehe 5 Novemba. Upande wa "Republican Party", mgombea
Richard Nixon
(pamoja na kaimu wake
Spiro Agnew
) aliwashinda mgombea wa "Democratic Party"
Hubert Humphrey
(pamoja na kaimu wake
Edmund Muskie
) na mgombea wa "American Independent Party"
George Wallace
(pamoja na kaimu wake
Curtis LeMay
).
Nixon akapata
kura
301, Humphrey 191 na Wallace 46 (pamoja na kura moja wa mchaguzi kutoka
North Carolina
aliyempigia kura Wallace badala ya Nixon).
Ramani
yaonyesha kura kwa kila
jimbo
.