Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jiji la Tokyo
(東京都) ni
mji mkuu
wa
Japani
. Takriban watu
milioni
12 huishi katika
jiji
hilo ambao ni sawa 10
%
ya Wajapani wote.
Rundiko la mji
lina wakazi milioni 35 na ni rundiko kubwa
duniani
.
Tokyo ni
kitovu
cha Japani upande wa
biashara
,
uchumi
na
siasa
.
Mahali pa jiji ni
tambarare
ya Kanto kando ya
hori
ya Tokyo.
Awali Tokyo iliitwa "Edo". Wakati ule
Kyoto
ilikuwa mji mkuu rasmi na mahali pa
Tenno
au
Kaisari
wa Japani. Edo ilikuwa mwanzoni
bandari
ndogo tu. Ilianza kukua baada ya kuwa makao makuu ya Ma
shogun
waliokuwa
viongozi
wa kijeshi katika Japani.
Katika
karne ya 19
Tenno Meiji
alihamisha mji mkuu kwenda Edo iliyoitwa "Tokyo" yaani "mji mkuu wa mashariki". Mji ulikuwa na tayari mwishoni mwa
karne ya 19
ulikuwa mji mkubwa wa pili duniani baada ya
London
.
Tokyo iliharibiwa na
moto
katika
historia
yake, pia na
matetemeko ya ardhi
na
mabomu
wakati wa
Vita Kuu ya Pili ya Dunia
. Ilijengwa upya na kukua kuwa jiji kubwa duniani.
Ilikuwa mahali pa
michezo
ya
Olimpiki
ya mwaka
1964
.
|
Makala hii kuhusu maeneo ya
Japani
bado ni
mbegu
.
Je unajua kitu kuhusu
Tokyo
kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|