Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sibusiso Zuma
|
|
Maelezo binafsi
|
Tarehe ya kuzaliwa
|
|
Mahala pa kuzaliwa
|
|
* Magoli alioshinda
|
Sibusiso Wiseman Zuma
(amezaliwa
Durban
,
KwaZulu-Natal
,
23 Juni
1975
) alikuwa
mwanakandanda
mtaalamu wa
Afrika Kusini
anayeichezea klabu ya kandanda ya Kideni Superliga inayoitwa FC Nordsjælland.
Zuma ilianza wasifi wake katika klabu za Afrika Kusini kama vile Mighty Pa, African Wanderers na
Orlando Pirates
. Mwezi Juni mwaka wa 2000, alijiunga na klabu ya Kideni ya FC København, ambapo alijiendeleza kama mchezaji. Aliisaidia klabu yake kushinda taji la ligi ya Kideni kwa mara yake ya pili na aliteuliwa kuingia katika “hall of fame” ya klabu kutokana na jitihada zake bora katika msimu wa 2004-05, na mwaka wa 2001 Zuma aliteuliwa katika nafasi ya 29 katika tuzo la mwanakandanda bora wa FIFA wa mwaka wa 2001. Baada ya miaka 5 ½ katika klabu ya FC København, Sibusiso Zuma aliuzwa kwa klabu ya Bundesliga, ambayo ni ya ligi ya Kijerumani, Arminia Bielefeld kwa kitita cha yuro milioni moja mnamo Julai 2005.
Mnamo 21 Juni 2008 Sibusiso Zuma alisainiwa na klabu ya Afrika Kusini ya
Mamelodi Sundowns
. Kisha aliachiliwa katika majira ya joto ya mwaka wa 2009 na mnamo Oktoba mwakwa wa 2009 alikuwa na kipindi cha majaribio na klabu ya FC Nordsjælland, [8] hatimaye kusainiwa na klabu hiyo.
Mnamo 16 Oktoba alisaini mkataba wa mwaka mmoja na klabu ya Kideni ya FC Nordsjælland. Mnamo 8 Novemba 2009 Zuma alifunga bao lake la kwanza la FC Nordsjælland katika ushinid wa klabu wa 1-0 dhidi ya SønderjyskE.
Yeye ameiwakilisha Afrika Kusini katika mechi 67. Aliicheza nchi yake katika
Kombe la Dunia la FIFA
la mwaka wa 2002. Zuma alikuwa nahodha wa timu ya kitaifa ya Afrika Kusini katika mashindano ya
Kombe la Mataifa ya Afrika
mwaka wa 2006.
Pia anajulikana kama "Zuma the Puma" kwa wafuasi wa klabu na "Puma" inaonekana kwa jesi lake badala ya "Zuma" katika mchezo wa komputa maarufu kama “video game” ijulikanayo kama
Pro Evolution Soccer 2009
.
Mnamo 25 Juni 2007 iliripotiwa kuwa Zuma alikuwa amehusika katika tukio katika nchi yake ya nyumba ya Afrika Kusini. Baada ya ugomvi mkali kulikuwa na madai kwamba alitishia kuwapiga risasi kundi la watu katika sherehe katika sehemu ya Kokstad. Polisi wa mtaa walichunguza hali hiyo na Zuma alizuiwa kuondoka nchini kwa muda, lakini hakuna mashtaka yalitolewa.
|
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Sibusiso Zuma
kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|