Shetani
(kwa
Kiebrania
??????
Satan
, kwa
Kigiriki
Σαταν??
Satanas
, kwa
Kilatini
Satanas
) ni
jina
linalomaanisha "Mpinzani"; "Mshtaki".
Shetani anajulikana pia kama
Ibilisi
(kutoka Kigiriki
Diabolos, -ou
, "Anayetenganisha"),
Mtawala wa giza
,
Mkuu wa ulimwengu huu
,
Belzebub
(jina la dhihaka kwa mungu
Baal
linalotafsiriwa "Bwana wa nzi"),
Belial
,
Lusiferi
(kutoka Kilatini
Lucifer
, "Mleta mwanga").
Kadiri ya
imani
ya
dini
mbalimbali, hasa zile zinazokubali
ufunuo
waliopewa
Waisraeli
, shetani ni
malaika
,
roho
, au
mungu mdogo
anayewakilisha
uovu
unaopingana na
Mungu
. Baadhi ya watu, kwa mfano
Wakristadelfiani
, hufundisha kwamba Shetani si nafsi hai, bali mfano tu wa
uovu
na
dhambi
.
Utendaji wake
Dhuluma
za shetani ni zile zote tunazoweza kuteswa naye, yaani:
- kushawishiwa,
- kupatwa na
- kupagawa.
Kuhusu hayo
neno
la
teolojia
ya
Kikristo
linaloyaangaza yote ni kwamba
kazi
ya shetani haivuki kamwe
hisi
zetu isiweze kutendeka moja kwa moja katika
akili
na
utashi
. “Mungu tu aliweza kuelekeza akili yetu kwenye ukweli wote na utashi wetu kwenye
wema
wote, na hatimaye kama lengo kuu kwake mwenyewe aliye wema mkuu. Kwa hiyo yeye tu anaweza kutenda moja kwa moja katika akili yetu na utashi wetu, kadiri ya elekeo la
umbile
ambalo mwenyewe aliliweka na analidumisha ndani ya vipawa hivyo” (
Thoma wa Akwino
). Mungu tu anapenya roho. Kwa
ruhusa
yake shetani anaweza akatushambulia akitenda katika
ubunifu
wetu, hisi zetu,
vitu
vya nje na
mwili
wetu ili kututia maovuni.
Tujihadhari tusizidhishe pande mbili tofauti: ama kumhusisha shetani na yale yanayotokana na
tabia
mbovu (
kiburi
na
tamaa
) au na
maradhi
; ama kutokubali kamwe uwepo wa athari yake wala kujali yale yanayofundishwa na
Maandiko
na
Mapokeo
matakatifu kwa Wakristo au na
misahafu
kwa
Waislamu
.
Kushawishwa
Watu wanapatwa na
vishawishi
kwa sababu mbalimbali, kama vile ubovu wa
moyo
na
mazingira
, lakini ikiwa ni vya ghafla, vya nguvu na vya kudumu na havielezeki kwa maradhi yoyote, inawezekana kuviona vimeathiriwa na shetani kwa namna ya pekee.
Kupatwa
Yeye anaweza akatenda: katika uwezo wa kuona kwa
maono
ya kuchukiza au ya kupendeza; katika uwezo wa kusikia kwa kusababisha
kelele
au kufanya yasikike maneno ya
kufuru
au ya
uzinifu
; katika uwezo wa kugusa kwa kupiga au kwa kupapasa
kimapenzi
. Pengine hayo hayatokei mwilini bali katika ubunifu au yanatokana na mhemko wa mishipa ya
neva
.
Kazi ya moja kwa moja ya shetani katika ubunifu,
kumbukumbu
na maono inaweza ikasababisha taswira zisizobanduka ingawa mtu anafanya juu chini azifukuze na ambazo zinaleta
hasira
,
chuki
,
pendo
la hatari au fadhaiko la kukatisha tamaa. Pengine wanaodhulumiwa hivyo wanahisi kwamba ubunifu wao ni kama umefungwa na
giza
nene na kwamba moyo wao unalemewa na
uzito
unaowakandamiza. Ni utovu wa
nguvu
ulio tofauti na ule unaotokana na kazi ya Mungu ambaye akijalia kuzama katika mafumbo anasababisha
tafakuri
karibu isiwezekane.
Adui
yake, akitamani kwa
wivu
kumuiga, anajitahidi kuchepusha matokeo ya kazi hiyo, hivi kwamba katika
matakaso ya Kimungu
mtu anajikuta pengine kati ya utendaji wa Mungu, unaomuelekeza
maisha ya Kiroho
yasiyotegemea zaidi hisi, na utendaji wa adui unaomsababishia kwa namna yake utovu wa nguvu ili kumchanganya.
Maria wa Yesu Msulubiwa
alipatwa na majaribu ambayo ni kati ya yale makubwa zaidi yanayoweza yakaendana na matakaso ya Kimungu na ambayo yanadhihirisha
ukweli
wa maneno ya
Yohane wa Msalaba
: “Ni vita vya wazi kati ya roho mbili… Mungu kadiri na jinsi anavyomvuta mtu anamruhusu shetani atende dhidi yake kwa namna hiyo… Pengine shetani anamtisha sana mtu: duniani hakuna teso la kufanana na hilo. Roho inaishirikisha roho hofu yake”.
Kupagawa
Katika kupagawa shetani anakaa mwilini mwa mhusika, badala ya kutokeza tu utendaji wake toka nje inavyotukia katika kupatwa naye. Akitenda hivyo toka ndani, hazuii tu utendaji wa
hiari
wa vipawa vya mtu, bali anasema na kutenda mwenyewe kupitia
viungo
vya mtu, bila huyo kuweza kumzuia na kwa kawaida hata kutambua. Shetani hamkalii mtu kama roho inavyohuisha mwili wake, bali kama
mota
ambayo kupitia mwili inatenda rohoni. Anatenda moja kwa moja katika viungo vya mwili vifanye matendo ya kila aina, na kwa njia yake anatenda katika vipawa kadiri vinavyotegemea mwili kwa kutenda kazi.
Wakati wa upeo wa hali hiyo kwa kawaida mhusika anapotewa na hisi yoyote ya mambo yanayomtokea, kwa sababu baadaye hakumbuki lolote isipokuwa mara mojamoja. Wakati wa
utulivu
ni kana kwamba shetani amejiondokea, ingawa pengine yanabaki maradhi ya kudumu ambayo
madaktari
wanashindwa kuyatibu.
Kwa kawaida kupagawa ni
adhabu
kuliko jaribu la kutakasa, lakini katika watu waliojitoa mhanga kwa ajili ya wakosefu hali hiyo inaweza ikaendana na
takaso la Kimungu la hisi
au
la roho
.
Dalili za kupagawa kweli
Ni kusema kwa
lugha
isiyojulikana au kumuelewa mtu anayeiongea; kuvumbua mambo ya mbali na ya
siri
; kuonyesha nguvu inayozidi ile ya kimaumbile ya mhusika, kulingana na
umri
na hali yake.
Dalili
hizo na nyinginezo, hasa zikipatikana nyingi kwa pamoja, zinatufanya tushuku mtu amepagawa. Kwa namna ya pekee zinashtusha ikiwa k.mf. mtu asiyejua Kilatini wala teolojia anakuja kusema Kilatini kwa ufasaha kuhusu masuala magumu ya teolojia.
Dalili nyingine ya kupagawa ni mtu kukasirika na kumkufuru Mungu kwa namna ya kutisha akiguswa kwa kitu kitakatifu au akiombewa kwa
sala
fulani. Dalili hiyo ni wazi zaidi ikiwa anaguswa au kuombewa bila yeye kujua, hivi kwamba itikio hilo lisiweze kutokana na hiari yake kwa ubaya au kwa kujifanya amepagawa.
Katika
umanyeto
wa hali ya juu yanatokea mambo ya namna hiyo, ingawa si kiasi cha kumfanya
mgonjwa
atoe
hoja
kwa lugha asiyoijua au juu ya suala asilolielewa. Tena shetani anaweza akasababisha maradhi ya akili au matukio ya nje yanayofanana nayo; anaweza vilevile kutumia maradhi yaliyopo na kumkatisha mgonjwa tamaa.
- Kufanya
toba
na kutakasa
dhamiri
kwa
kuungama
vema.
- Kupokea
ekaristi
mara nyingi kufuatana na
shauri
la
padri
mwenye
busara
na mwanga. Kadiri tulivyo safi na wenye toba shetani hana uwezo juu yetu, na ekaristi takatifu inatupatia
Yesu
, yule ambaye alitustahilia
neema
na kumshinda shetani. Hata hivyo komunyo iruhusiwe tu wakati wa utulivu.
- Kuomba mara nyingi
huruma ya Mungu
kwa sala na
mfungo
.
- Kukimbilia kwa
tumaini
jina takatifu la Yesu
na kutumia kwa
imani
kubwa
visakramenti
, hasa
ishara ya msalaba
na
maji ya baraka
.
- Hatimaye kwa
ukombozi
wa waliopagawa yamewekwa
mazinguo
kutokana na
mamlaka
ya kufukuza mashetani ambayo Yesu
Kristo
ameliachia
Kanisa
. Lakini mazinguo makuu yanaweza kufanywa na mapadri wale tu walioteuliwa na kupewa ruhusa maalumu na
askofu
wa
jimbo
.
Marejeo