Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rais Trump
wa
Marekani
na
Kim Jong Un
wa
Korea Kaskazini
walikutana
Singapur
mwaka
2018
katika jaribio la kubadilisha sera za kigeni kati ya mataifa yao.
Sera za kigeni
ya
nchi
(pia inaitwa
sera ya mahusiano ya kimataifa, siasa ya nje
;
kwa Kiingereza: foreign policy)
ni jumla ya matendo, matamko na mipango ya nchi vinavyolenga kuendeleza uhusiano wake na nchi nyingine, pamoja na jumuiya na mashirika vya nchi za nje kuhusu
uchumi
,
siasa
,
jamii
na
jeshi
.
Sera za kigeni zinabuniwa ili kusaidia kulinda
maslahi
ya
taifa
,
usalama wa taifa
, malengo ya
kiitikadi
, na
mafanikio
ya kiuchumi. Hii inaweza kufanyika kama matokeo ya ushirikiano wa
amani
na mataifa mengine, au kwa njia za kutisha hadi kutumia nguvu ya kijeshi.
Kwa kawaida sera ya kigeni huongozwa na
waziri mkuu
na
waziri wa mambo ya nje
. Katika baadhi ya nchi
bunge
pia lina
jukumu
kiasi la kuzisimamia.
Katika nchi mbalimbali, hasa zenye
Serikali ya kiraisi
, mkuu wa nchi ana jukumu kwa sera za kigeni, wakati mkuu wa
serikali
hasa anahusika na sera ya ndani.
Nadharia ya mahusiano ya kimataifa
[
hariri
|
hariri chanzo
]
Taaluma
inayoshughulika na
utafiti
wa mahusiano ya kigeni hujulikana kama
uchambuzi wa sera za kigeni
(
Foreign Policy Analysis
).