Seiwa ( 850 – 31 Desemba , 878 ) alikuwa mfalme mkuu wa 56 ( Tenno ) wa Japani . Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Korehito , na alikuwa mwana wa nne wa Tenno Montoku . Mwaka wa 858 alimfuata babake, na kuwa mfalme hadi kujiuzulu mwaka wa 876. Aliyemfuata kama Tenno ni mwana wake, Yozei .