Samweli
(kwa
Kiebrania
: ?????????
??mu?el
, maana yake labda ni "Anayemsikiliza Mungu";
1070
-
1000 KK
hivi) ni
mtu
muhimu wa
Historia ya wokovu
ya
Agano la Kale
.
Katika
Biblia
anatajwa kama
mwamuzi
wa mwisho na mkuu kuliko wote, tena kama
nabii
tangu
utotoni
. Ndiye
mwanzilishi
wa
ufalme wa Israeli
kwa kuwa kwa agizo la
Mungu
alimpaka
mafuta
Sauli
awe
mfalme
wa
taifa
lake, tena, baada ya huyo kukataliwa kwa ukaidi wake, alimpaka vilevile
Daudi
, ambaye kutoka uzao wake akaja kutokea
Masiya
[1]
.
Habari zake zinasimuliwa katika
Vitabu vya Samweli
.
Kanisa Katoliki
na
madhehebu
mbalimbali za
Ukristo
vinamheshimu kama
mtakatifu
hasa tarehe
20 Agosti
[2]
.
Vitabu
viwili vya
Biblia ya Kikristo
vinaitwa kwa
jina
la mtu huyo, ambaye kwa njia yake
Israeli
ilianza kuwa na
umoja
zaidi na hatimaye kuwa
ufalme
. Badala ya kila
kabila
kujitegemea,
yote 12
yalikubaliana yawe na
kiongozi
mmoja wa kudumu ambaye
cheo
chake kirithiwe na
mwanae
. Kwa umoja huo waliweza kushinda ma
adui
wao wengi.
Vitabu hivyo vimekusanya
kumbukumbu
zote kuhusu mwanzo wa ufalme (
1070
-
972
hivi K.K.), yaani kuhusu Samweli mwenyewe na
wanaume
wawili aliowapaka
mafuta
watawale Israeli kwa niaba ya
Mungu
: kwanza
Sauli
, halafu
Daudi
. Kumbukumbu hizo zilikuwa nyingi na tofauti, hivyo tunakuta humo tata nyingi kuliko katika vitabu vingine vyote vya
Biblia
. Hasa mna
hoja
za kukubali
mfumo
wa ufalme na hoja za kuukataa.
Ukuu wa Samweli ulidokezwa kwanza na
uzazi
wake wa ajabu, kwa kuwa
mama
yake,
Ana
, alikuwa tasa akampata baada ya
kusali
na kuweka
nadhiri
(1Sam 1). Hivyo baada ya miaka michache alihamia
Shilo
kwenye
sanduku la agano
kama
mtumishi
wa
kuhani
Eli
.
1Sam 3 inasimulia
wito
wake: akiwa amelala karibu na sanduku hilo akaamshwa na
Mungu
mara tatu mpaka akafundishwa na Eli kumtambua na kumuitikia Mungu. Hapo akamtabiria Eli
adhabu
kali, na hivyo Israeli ikajua kuwa amefanywa nabii wa Bwana.
Samweli aliwaamua Waisraeli kwa kuwakomboa
mikononi
mwa
Wafilisti
(1Sam 7), lakini ni muhimu hasa kwa kuwaanzishia ufalme kwa kuwaweka wakfu kwanza Sauli halafu Daudi. Kadiri ya 1Sam 8, yeye na Mungu hawakupendezwa na jinsi Waisraeli wengi walivyotaka kuiga mtindo wa mataifa yote: Samweli aliwaangalisha kuhusu matatizo na
unyonyaji
wa wafalme, naye Mungu aliona katika
ombi
hilo
uasi
ambao Waisraeli wanamkataa asiwatawale tena, lakini akamuagiza Samweli awakubalie.
Ukweli
ni kwamba mfalme aliwekwa
wakfu
kwa Mungu kama
mwakilishi
wake akitakiwa kutimiza
matakwa
yake, hasa kwa kusikiliza anamuambia nini kwa
kinywa
cha manabii wake. Ndiyo sababu Samweli alizidi kumuelekeza Sauli, na hatimaye akamkataa kwa
ukaidi
wake.
Mabishano
kati ya Samweli na Sauli ni mwanzo wa mabishano yote kati ya manabii na wafalme ambao hawakutaka kumtii Mungu, na hatimaye wakadhulumu na kuua manabii wake.
Mamlaka
ya
neno la Mungu
lililoletwa na nabii ilitakiwa kuwa juu ya mamlaka ya
serikali
na
nguvu
ya
kijeshi
alivyokuwa navyo mfalme. Lakini mara nyingi wafalme, kwa kujivunia cheo chao, walishindwa kumnyenyekea nabii wa Mungu, wakaona afadhali kufuata manabii wengine wengi waliosema
uongo
ama kwa kudanganywa na matarajio yao ama kwa kujipendekeza kwa mfalme na kwa
taifa
lote.
"Nena, Bwana, kwa kuwa mtumishi wako anasikia".
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
|
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Samweli
kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|