Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rosa Parks
|
![](//upload.wikimedia.org/wikipedia/sw/thumb/8/84/Rosaparksarrested.jpg/225px-Rosaparksarrested.jpg)
|
Amekufa
|
24 Oktoba 2005
|
Nchi
|
Marekani
|
Kazi yake
|
Mwana arakati wa marekani
|
Rosa Louise McCauley Parks
(
4 Februari
1913
?
24 Oktoba
2005
) anakumbukwa kwa uamuzi wake wa kukataa kumpisha kiti Mmarekani Mweupe kama alivyodaiwa na dereva wa basi. Uamuzi wake huo hapo mwaka
1955
ulipelekea mzozo uliosababisha Mgomo wa Mabasi wa Montgomery na kuchangia katika Vuguvugu la Haki za Kiraia Marekani. Baada ya kitendo chake cha kukataa kumpa mtu mweupe kiti ndani ya basi na Mgomo wa Montgomery uliodumu kwa mwaka, Mahakama ya Marekani ilitamka kuwa sheria za ubaguzi ndani ya mabasi huko Alabama na Montgomery zilikiuka katiba.