Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
"
Regina caeli
" (tamka: re?d?ina ?t?eli; maana yake
Malkia wa Mbingu
)ni
antifona
inayotumika kumuelekea
Bikira Maria
katika
Kanisa la Kilatini
wakati wa Pasaka
, kuanzia
Dominika
ya
Ufufuko wa Yesu
hadi
Pentekoste
.
Katika
siku
hizo
hamsini
ndiyo antifona pekee inayotumika kumalizia
Sala ya mwisho
ya
Liturujia ya Vipindi
[2]
lakini pia inashika nafasi ya
sala
ya
Angelus
(inayofanyika mara tatu kwa siku:
asubuhi
,
adhuhuri
na
jioni
).
- Regina caeli, laetare, alleluia;
- Quia quem meruisti portare, alleluia,
- Resurrexit, sicut dixit, alleluia:
- Ora pro nobis Deum, alleluia.
[3]
- Malkia wa mbingu, furahi, aleluya;
- Kwani uliyestahili kumchukua, aleluya,
- Amefufuka, alivyosema, aleluya:
- Utuombee kwa Mungu, aleluya.
[4]
Mtunzi
wa Regina caeli hajulikani. Kimaandishi inapatikana katika
kitabu cha antifona
cha
mwaka
1200
hivi kinachotunzwa katika
Basilika la Mt. Petro
, huko
Vatikani
,
jijini
Roma
.
[5]
Wikimedia Commons ina media kuhusu: