Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Parokia
ni muundo mmojawapo wa zamani sana wa
Kanisa Katoliki
, ambao umuhimu wake unatokana na kwamba ni sehemu ya
jimbo
(
dayosisi
) unapofanyika
uchungaji
wa kila
siku
chini ya
kasisi
anayemwakilisha
Askofu
.
Kiini cha
maisha
ya parokia ni
adhimisho
la
Ekaristi
siku ya
Jumapili
, ambapo
jumuia
nzima ya
Kikristo
ya eneo husika inakusanyika isikilize
Neno la Mungu
, imsifu
Mungu
na
Kumega mkate
.
Jina
hilo lilianza kutumika katika
karne III
kutokana na
neno
la
Kigiriki
παρоικια (=ujirani) linalotumika katika
tafsiri
ya
Biblia
ya
Septuaginta
kwa maana ya
kukaa ugenini
.
Kanuni
515 za
Sheria za Kanisa la Kilatini
inasema, "Parokia ni
jumuia
rasmi ya waamini ambayo imeundwa kwa namna ya kudumu ndani ya
Kanisa maalumu
na imekabidhiwa kichungaji kwa
paroko
kama
mchungaji
wake chini ya
mamlaka
ya
Askofu
wa jimbo. Ni juu ya Askofu wa jimbo tu kuanzisha, kufuta na kubadilisha parokia; lakini asizianzishe, asizifute wala asizibadilishe sana kabla hajapokea maoni ya
Halmashauri ya mapadri
. Parokia iliyoundwa kihalali papo hapo ina
hadhi
ya
nafsi ya kisheria
".
Mbali ya
Kanisa Katoliki
, ambalo lina
mtandao
mkubwa zaidi wa parokia
duniani
kote,
Waorthodoksi
,
Waanglikana
,
Walutheri
na
Wakristo
wengine kadhaa wanatumia muundo wa namna hiyo, ingawa mikazo ni tofauti, kulingana na
teolojia
yao.
|
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Parokia
kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|