한국   대만   중국   일본 
Papa Paskali I - Wikipedia, kamusi elezo huru Nenda kwa yaliyomo

Papa Paskali I

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mt. Paskali I.

Papa Paskali I alikuwa Papa kuanzia tarehe 25 Januari 817 hadi kifo chake mnamo Februari / Mei 824 [1] . Alitokea Roma , Lazio , Italia [2] .

Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Paskali Massimi, mwana wa Bonosus [3] .

Alimfuata Papa Stefano IV akafuatwa na Papa Eugenio II .

Kabla ya kuchaguliwa Papa alikuwa abati wa monasteri iliyohudumia waliofika mjini Roma kwa hija [4] . Kwa kuwa hakusubiri kupata uthibitisho wa kaisari Pius Mtawa , alimtuma balozi kwake [5] naye akarudi na hati Pactum cum Paschali pontifice , ambamo kaisari alimpongeza, alithibitisha mamlaka ya Papa juu ya Dola la Papa , na kuhakikisha siku za mbele uchaguzi wa Mapapa hautaingiliwa na serikali tena. [6] Wanahistoria wana wasiwasi kuhusu hati hiyo kuwa halisi. [7] Kwa vyovyote, baada ya Papa Paskali I kumtia taji la kifalme Lotari I , mwana wa Pius, mahusiano yalizidi kuharibika.

Papa Paskali I alipokea wamonaki wengi kutoka Dola la Roma Mashariki waliokimbia dhuluma ya serikali kuhusu picha takatifu [8] , akawapa kazi ya kupamba makanisa aliyoyajenga au kuyakarabati [6] [9] pamoja na kuwatetea kwa maandishi yake.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu [10] [5] , hasa tarehe 11 Februari [11] [12] au 14 Mei [13] [14] .

Tazama pia [ hariri | hariri chanzo ]

Maandishi [ hariri | hariri chanzo ]

Tanbihi [ hariri | hariri chanzo ]

  1. https://www.vatican.va/content/vatican/en/holy-father.index.html#holy-father
  2. https://www.vatican.va/content/vatican/en/holy-father.index.html#holy-father
  3. Goodson, 2010, p. 9 & n.13.
  4.  One or more of the preceding sentences incorporates text from a publication now in the public domain Kirsch, Johann Peter (1911). "Pope Paschal I" . In Herbermann, Charles. Catholic Encyclopedia . 11 . Robert Appleton Company . http://www.newadvent.org/cathen/11514a.htm .
  5. 5.0 5.1 O'Brien, Richard P. (2000). Lives of the Popes . New York: Harper Collins. ku.  132-133 . ISBN   0-06-065304-3 .
  6. 6.0 6.1 John N.D. Kelly, Gran Dizionario Illustrato dei Papi , p. 271
  7. Claudio Rendina, I papi , p. 256
  8. "Saint Paschal I | pope" . Encyclopedia Britannica (kwa Kiingereza) . Iliwekwa mnamo 2021-06-01 .
  9. Goodson, 2010, p. 3.
  10. "CATHOLIC ENCYCLOPEDIA: Pope Paschal I" . www.newadvent.org . Iliwekwa mnamo 2021-06-01 .
  11. Martyrologium Romanum
  12. Zeno. "Lexikoneintrag zu ≫Paschalis I, S. (2)≪. Vollstandiges Heiligen-Lexikon, Band 4. ..." www.zeno.org (kwa Kijerumani) . Iliwekwa mnamo 2021-06-01 .
  13. "14.05: Memoria di San Pasquale I, Papa e Patriarca di Roma, che confessa la retta fede di fronte e contro l'eresia iconoclasta (verso l'anno 824)" . www.ortodossia.it . Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-11-07 . Iliwekwa mnamo 2021-08-12 . {{ cite web }} : More than one of |accessdate= na |access-date= specified ( help )
  14. " 98. ПАСХАЛИЙ I ", Церковно-Научный Центр "Православная Энциклопедия" . (ru)  

Marejeo [ hariri | hariri chanzo ]

  • Goodson, Caroline J. 2010. The Rome of Pope Paschal I: Papal Power, Urban Renovation, Church Rebuilding and Relic Translation, 817?824 . Cambridge University Press.
  • John N.D. Kelly, Gran Dizionario Illustrato dei Papi , Edizioni Piemme S.p.A., 1989, Casale Monferrato (AL), ISBN 88-384-1326-6
  • Claudio Rendina, I papi , Ed. Newton Compton, Roma, 1990

Viungo vya nje [ hariri | hariri chanzo ]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu .
Je, unajua kitu kuhusu Papa Paskali I kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari .