Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ozoni
(kwa
Kiingereza
:
ozone
, pia
trioxygen
) ni
molekuli
yenye
alama
ya O
3
inayofanywa na
atomi
tatu
za
oksijeni
.
Inaonekana kama
gesi
ya
buluu
yenye
harufu
kali. Inatokea katika
matabaka
ya juu ya
angahewa
ambako
mnururisho wa urujuanimno
unapasua molekuli za O
2
.
Inatokea pia katika
mazingira
ya
mashine
kama ya
fotokopi
zinazotumia
volteji
ya juu.
Si molekuli thabiti, hivyo inasambaratika tena baada ya
muda
.
Ozoni hupatikana kwa viwango vidogo vya
ppm
0.6 katika angahewa. Kiasi kikubwa kipo kwenye
tabakastrato
baina ya
kilomita
10 hadi 50 juu ya uso wa ardhi. Tabaka hili lenye ozoni linafyonza
asilimia
kubwa ya
mnururisho wa urujuanimno
(93-99
%
) ulio hatari kwa
viumbehai
duniani
.
Katika matabaka ya chini ya angahewa ozoni ni
sumu
kwa viumbehai ikitokea kwa viwango juu ya ppm 0.1. Kwa
binadamu
inaweza kukera
pua
na
koo
pamoja na kuleta
kichefuchefu
. Kuathiriwa kwa muda mrefu kunaweza kuleta kufura kwa
mapafu
[1]
.
Ppm 0.100 ni kiwango cha juu kinachoruhusiwa ndani ya
karakana
,
viwanda
au
ofisi
katika nchi kama
Uingereza
,
Japani
,
Ufaransa
,
Uholanzi
na
Ujerumani
.
Kutokana na nguvu yake ya kuoksidisha, ozoni hutumiwa kwa madhumuni mbalimbali:
- kusafisha
maji
: ozoni inaua
bakteria
na
algae
hivyo hutumiwa katika mchakato wa kusafisha maji kwa matumizi ya viwandani na maji ya kunywa
- ↑
Ozone backround information, Effects on humans
, tovuti ya National Center for Biotechnology Information, iliangaliwa Mchi 2019
|
Makala hii kuhusu mambo ya
kemia
bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Ozoni
kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|