Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Numidia
ni eneo la kihistoria katika
Afrika ya Kaskazini
. Leo hii ni sehemu ya nchi za
Tunisia
na
Aljeria
.
Ilijulikana katika karne za
KK
kama eneo la
Wanumidia
waliokuwa tawi la
Waberberi
.
Baada ya kufika kwa
Wafinisia
waliounda ma
koloni
kama
Karthago
na kutawala
pwani
, Wanumidia walisukumwa kwenda
milima
ya
Atlasi
na mitelemko yake.
Mnamo mwaka
200
wakati wa
vita ya pili ya Waroma dhidi Karthago
Massinissa aliunda ufalme wa Numidia iliyotawala nchi kati ya Karthago na ufalme wa
Mauritania
upande wa magharibi.
Mtoto wake Yugurtha aliendesha vita kali dhidi ya Roma lakini alishindwa. Wakati wa karne ya kwanza KK Numidia ilikuwa
nchi lindwa
chini ya Roma.
Mfalme wa mwisho wa Numidia alishiriki katika vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Waroma upande wa
Pompeio
lakini alishindwa na
Caesar
.
Tangu mwaka
46
BK
nchi ikawa jimbo la
Dola la Roma
kwa jina la "Numidia Cirtensis". Numidia ilistawi kiuchumi na kiutawala. Miji mingi ilianzishwa na kuendelea vizuri.
Baada ya mwaka
400
kuna taarifa ya ma
askofu
123 kutoka Numidia waliokutana kwenye
sinodi
za Karthago. Wakati ule askofu alipatikana tu katika mji wenye umuhimu fulani na idadi hii ni
dalili
ya maendeleo inayoonekana leo hii kutokana na maghofu mengi.
Tangu kuingia kwa
Wavandali
hali ya uchumi ilizorota. Ma
shamba
hayakulimwa tena na
jangwa
lilipanuka.
Kuja kwa
Waarabu
hakusaidia kushuka kwa hali ya maisha kulingana na kale za Waroma.