Siasa
ni njia ya kufanya
maamuzi
katika ngazi mbalimbali za
jamii
, kama vile
mji
,
taifa
, au hata
dunia
nzima (
siasa ya kimataifa
).
Sehemu muhimu ya siasa ni
majadiliano
kati ya
watu
mbalimbali wenye
nguvu
au
mamlaka
.
Katika
demokrasia
kila mtu ana kiasi fulani cha nguvu, kwa hiyo siasa ya demokrasia ina maana ya watu wote kuchangia maamuzi.
Hapa chini, mifumo mbalimbali ya kisiasa huelezwa kifupi:
Utawala wa Kifalme
ni mfumo wa uongozi unaompa mamlaka ya
dola
na ya
serikali
Mfalme
. Katika mfumo huu
madaraka
hurithiwa na mtu wa
familia
ya kifalme.
Utawala wa Kiimla
ni mfumo wa uongozi unaotoa madaraka yasiyo na mipaka kwa
kiongozi
. Katika utawala huu watu binafsi hawana
haki
na
uhuru
katika maamuzi.
Utawala finyu
ni mfumo unaowapa wachache kati ya wengi nguvu za maamuzi katika dola na serikali. Nafasi ya wachache hawa hutokana na
haiba
na
uwezo
wao ki
uchumi
, ki
jamii
, ki
jeshi
au kutokana na mafanikio yao katika nyanja mbalimbali za maisha. Mfumo huu ni nadra sana siku za hivi karibuni. Pia waweza kuitwa utawala wa ma
kabaila
.
Utawala wa Umma
ni utawala unaotokana na jamii kuamua misingi ya kujiongoza, hivyo unatoa fursa ya madaraka kwa
umma
moja kwa moja au kutokana na kuwakilishwa. Mfumo huu wa utawala hujulikana kama demokrasia na umegawanyika katika sehemu zifuatazo:
Demokrasia Chama
ni aina ya demokrasia ya kura. Inashirikisha watu wote kuwa wanachama.
Demokrasia Baguzi
ni aina ya demokrasia inayojikita katika kulinda nguvu za kiuchumi zaidi.
Demokrasia Duni
ni aina ya demokrasia inayotokana na makundi ya watu na kisha kupitia makundi hayo watu kuunda serikali mfano:
chama
- serikali.
Demokrasia Endelevu
ni aina ya demokrasia inayotoa
fursa
ya
usawa
na kupinga ma
tabaka
katika jamii.
Demokrasia Shirikishi
katika aina hii ya demokrasia wachache hupewa
dhamana
na wengi katika
uwakilishi
wa jamii katika maamuzi.
Wachache huchaguliwa na wengi kwa njia ya demokrasia huru na haki kwa kufuata Katiba ya nchi hiyo. Mfano: Wa
bunge
huwakilisha wananchi wao katika kuleta maendeleo na kuishauri serikali juu ya maendeleo ya nchi.