Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Basilika
la
Mtakatifu Yohane
huko Laterano ambamo mtaguso ulifanyika.
Mtaguso wa tatu wa Laterano
uliitishwa na
Papa Aleksanda III
(
1159
-
1181
) ufanyike huko
Roma
mwaka
1179
, kutokana na
Amani ya Venezia
kati ya
Kaisari
Federiko I wa Ujerumani
na
Lega Lombarda
ya
Italia kaskazini
.
Unahesabiwa na
Kanisa Katoliki
kama
mtaguso mkuu
wa
kumi na moja
.
Ulihudhuriwa na viongozi wa
Kanisa
300 na kufanyika katika vikao vitatu, tarehe
5 Machi
,
7 Machi
na
19 Machi
1179
.
Ulijadili masuala mbalimbali na kuyatungia kanuni 27 na kutangua zile zilizotolewa na
antipapa Paskali III
. Kati ya maamuzi muhimu zaidi, mmojawapo ulihusu
uchaguzi
wa
Papa
, ukidai
thuluthi
mbili za kura za
makardinali
wote, bila ya kutofautisha haki za makundi yao matatu.
|
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Mtaguso wa tatu wa Laterano
kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|