Mtaguso wa nne wa Konstantinopoli
ni jina linalotumiwa na
Wakristo
kwa namna tofauti, kadiri wanavyokubali au kukataa uhalali na uekumeni wa mitaguso fulanifulani.
Kanisa Katoliki
linahesabu kuwa
Mtaguso mkuu
wa
nne
ule uliofanyika tangu tarehe
5 Oktoba
869
hadi
28 Februari
870
.
Uliitishwa na
Kaisari
Basili I wa Bisanti
na
Papa Adrian II
(
867
-
872
) kwa sababu mwisho wa
ikonoklastia
katika
sinodi
ya mwaka
843
ulikuwa umeacha athari kubwa katika
Kanisa
la Mashariki
.
Patriarki
Metodi wa Konstantinopoli
(843-
847
) alijitahidi kutuliza pande zote, lakini hakufaulu.
Alipofariki, malkia Teodora, akitawala kwa niaba ya mtoto
Mikaeli III wa Bisanti
alilazimisha nafasi yake ishikwe na
Ignas I
(847-
858
),
mmonaki
mwenye msimamo mkali, ambaye hatimaye aliondoshwa.
Badala yake alichaguliwa
mlei
msomi
Fosyo
ambaye kwa siku chache alipewa
daraja
na kutawazwa, lakini kufikia Februari
859
lililotea farakano kati ya waliomkubali yeye na waliomkubali Ignas I.
Ndipo Fosyo alipojitahidi kuungwa mkono na
Papa Nikolaus I
(
858
-
867
), ambaye kwanza alimkubali pamoja na pendekezo la Kaisari Mikaeli III la kuitisha mtaguso uliofanyika
Konstantinopoli
kati ya Aprili na Agosti
861
wakihudhuria maaskofu zaidi ya 300.
Papa
hakupendezwa na maamuzi ya mtaguso huo, akashindana na Kaisari kimaandishi kwa sababu za ki
utamaduni
na za ki
siasa
pia.
Hapo Fosyo alipata nguvu dhidi ya Papa akaitisha mtaguso uliovunja
umoja
kati ya Makanisa ya Mashariki na yale ya Magharibi mwaka
867
, akithubutu kwa mara ya kwanza kumhukumu Papa kama
mzushi
na kutaka kumuondoa madarakani.
Kumbe Kaisari mpya alimrudisha Ignas I kuwa Patriarki na pamoja naye akamuomba Papa atume mabalozi kwa mtaguso mwingine wa kufanyika Konstantinopoli.
Mtaguso ulipoanza tarehe
5 Oktoba
869 walikuwepo tu maaskofu wakuu 5 na maaskofu wengine 7, lakini walikuwepo mabalozi wa Mapatriarki wa Antiokia na Yerusalemu (wale wa Aleksandria walifika baadaye).
Waliokuwa upande wa Fosyo walikubaliwa kuhudhuria kuanzia tarehe
7 Oktoba
wakamtetea sana dhidi ya msimamo wa
Papa
, lakini wakashindwa na kutengwa (
29 Oktoba
).
Baada ya miezi mitatu mtaguso uliendelea tarehe
12 Februari
870, wakiwepo maaskofu 67 walioongezeka tena hadi kufikia 103 siku ya mwisho (
28 Februari
), lilipotolewa tamko la imani pamoja na kanuni 26 kuhusu teolojia na sheria, bila ya kutoa mafundisho mapya. Pamoja na idadi yenyewe kutokuwa kubwa sana, ni muhimu kwamba walikuwepo
maaskofu wakuu
37 kati ya 40.
Kwa kuwa mtaguso huu haukukubaliwa sana huko Konstantinopoli (hasa baada ya Fosyo kurudia Upatriarki mwaka
877
), na pande mbili zilishindwa zaidi na zaidi kuelewana, uliitishwa mtaguso mwingine, ambapo wafuasi wa Fosyo walikuwa ndio wengi.
Baadhi ya Waorthodoksi wanahesabu mtaguso huo mpya (
879
-
880
), uliofuta maamuzi dhidi ya Fosyo, kuwa wa kiekumeni na kuukataa ule wa miaka 10 ya nyuma. Lakini wengine hawaukubali kuwa wa kiekumeni kwa sababu haukutoa mafundisho ya imani.
Ingawa wajumbe wa
Papa Yohane VIII
(
872
-
882
) walikubali kwanza maamuzi wa mtaguso huo ili kudumisha amani, na labda hata yeye mwenyewe, waandamizi wake waliukataa, na Fosyo mwenyewe aliondoshwa tena mwaka
886
.
|
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Mtaguso wa nne wa Konstantinopoli
kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|