Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mtaguso wa Vienne
(
1311
-
1312
) unahesabiwa na
Kanisa Katoliki
kama
mtaguso mkuu
wa
kumi na tano
.
Mtaguso
huu ulifanyika
Vienne
(
Ufaransa
) baada ya mashindano kati ya
Papa Boniface VIII
(
1294
-
1303
) na
mfalme
wa Ufaransa
Filipo IV
.
Hatimaye mwaka 1309 mwandamizi wake,
Papa Klementi V
(
1305
-
1314
), alikubali kubaki
Avignon
(leo nchini Ufaransa) karibu na himaya ya mfalme huyo. Mapapa walibaki huko hadi mwaka
1377
, waliporudi
Roma
.
Kwa shinikizo la mfalme, Papa alitoa hati
Regnans in excelsis
(
12 Agosti
1308
) ili kuitisha mtaguso mkuu huko
Vienne
tarehe
1 Novemba
1310
, kwa lengo la kujadili mada 4:
- suala la Wahekalu;
- vita vya msalaba
;
- hali ya
imani
na
Kanisa
kwa jumla;
- urekebisho
wa Kanisa.
Mtaguso wenyewe na maamuzi yake
[
hariri
|
hariri chanzo
]
Mtaguso ulichelewa kuanza hadi tarehe
16 Oktoba
1311
, walipokuwepo washiriki 170 hivi, ambao kati yao Wafaransa walikuwa zaidi ya thuluthi moja. Wengine walizuiwa na mfalme wa Ufaransa.
Vikao rasmi vikawa vitatu hadi Machi 1312.
Mtaguso uliamua kufuta shirika lao kama alivyopenda mfalme, bila ya kulifanyia utafiti wala kulitolea hukumu.
Mtaguso uliamua kuvianza upya na kwa ajili hiyo kutoza
zaka
kwa miaka
sita
, lakini mfalme alijitwalia hizo
pesa
bila ya kutekeleza
ahadi
yake ya kuongoza vita hivyo.
Mtaguso ulijadili baadhi ya mafundisho hasa ya makundi kadhaa ya
watawa
, lakini uamuzi ulichukuliwa baadaye tu.
Mtaguso ulidai haki za Kanisa ziheshimiwe na
serikali
za nchi. Pia ulijadili kirefu mahusiano ya ndani, hasa kati ya ma
askofu
, ma
paroko
na watawa.
|
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Mtaguso wa Vienne
kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|