Mtaguso mkuu
ni mkutano mkuu wa ma
askofu
kutoka pande zote za dunia na waamini wengine kadhaa ambao unafanyika kwa nadra sana katika
Ukristo
.
Ona makala kuu:
Mitaguso ya kiekumene
Mitaguso ya kiekumene
(kutoka
Kigiriki
oικουμ?νη
oikumene
yaani
dunia inayokaliwa na watu
) ni jina linalotumika hasa kwa mikutano saba ya namna hiyo iliyofanyika kati ya mwaka
325
hadi
787
upande wa mashariki wa
Dola la Roma
(ulioendelea baadaye kama Milki ya
Bizanti
).
Orodha yake ni kama ifuatavyo:
1.
Mtaguso wa kwanza wa Nisea
(mwaka 325)
2.
Mtaguso wa kwanza wa Konstantinopoli
(
381
)
3.
Mtaguso wa Efeso
(
431
)
4.
Mtaguso wa Kalsedonia
(
451
)
5.
Mtaguso wa pili wa Konstantinopoli
(
553
)
6.
Mtaguso wa tatu wa Konstantinopoli
(
680
-
681
)
7.
Mtaguso wa pili wa Nisea
(787)
Mitaguso hiyo, iliyofanyika wakati wa
Mababu wa Kanisa
, ilitoa maamuzi ya msingi juu ya mafundisho ya
imani
na
sheria za Kanisa
yaliyokuwa muhimu kwa maendeleo ya Ukristo ya baadaye.
Mitaguso
hiyo saba inakubaliwa hasa na
Kanisa Katoliki
na
Waorthodoksi
, kutokana na msisitizo wao wa
mapokeo
na wa
mamlaka ya kufundisha
ya waandamizi wa
Mitume
.
Makanisa ya kale ya mashariki
hukubali mitaguso mitatu ya kwanza tu, na
Kanisa la Asiria
ile miwili ya kwanza. Kukataa maamuzi ya mitaguso iliyofuata ndiyo sababu ya mafarakano yao.
Madhehebu kadhaa ya Kiprotestanti (hasa
Walutheri
,
Waanglikana
,
Wamethodisti
,
Wamoraviani
) yanakubali mitaguso hiyo kadiri inavyolingana na uelewa wao wa
Biblia
.
Hivyo Waprotestanti wengi wanashikilia imani juu ya
Yesu Kristo
, juu ya
Roho Mtakatifu
na juu ya
Utatu
mtakatifu kama ilivyofundishwa rasmi katika mitaguso ya kwanza.
Mitaguso ya baadaye katika Kanisa Katoliki
[
hariri
|
hariri chanzo
]
Kutokana na umuhimu wa mitaguso mikuu kwa Kanisa Katoliki na kwa Waorthodoksi, mikutano mikuu ya maaskofu iliendelea kufanyika ikatazamwa pengine kama mitaguso ya kiekumene.
Yafuatayo ni mitaguso mikuu inayohesabiwa katika kanisa katoliki. Karibu yote ilifanyika katika milenia ya pili magharibi (
Italia
,
Ufaransa
na
Ujerumani
wa leo):
8.
Mtaguso wa nne wa Konstantinopoli
(
869
-
870
)
9.
Mtaguso wa kwanza wa Laterano
(
1123
)
10.
Mtaguso wa pili wa Laterano
(
1139
)
11.
Mtaguso wa tatu wa Laterano
(
1179
)
12.
Mtaguso wa nne wa Laterano
(
1215
)
13.
Mtaguso wa kwanza wa Lyon
(
1245
)
14.
Mtaguso wa pili wa Lyon
(
1274
)
15.
Mtaguso wa Vienne
(
1311
-
1312
)
16.
Mtaguso wa Kostansa
(
1414
-
1418
)
17.
Mtaguso wa Firenze
(
1439
-
1445
)
18.
Mtaguso wa tano wa Laterano
(
1512
-
1517
)
19.
Mtaguso wa Trento
(
1545
-
1563
)
20.
Mtaguso wa kwanza wa Vatikano
(
1869
-
1870
)
21.
Mtaguso wa pili wa Vatikano
(
1962
-
1965
)
Mitaguso mikuu ya kwanza ilifanyika hasa ili kubainisha katika mafundisho yaliyogongana yapi yanalingana na imani sahihi. Mwisho wake ulikuwa kutangaza dogma fulani na kutenga na Kanisa watakaokataa kuiamini na watakaofundisha tofauti.
Kumbe mitaguso iliyofanyika baada ya farakano la mwaka 1054 kati ya
Kanisa la Mashariki
na
Kanisa la Magharibi
, pamoja na kulenga umoja uliovunjika na kufundisha dogma mpya, ilishughulikia zaidi urekebisho wa Kanisa katika ngazi na nyanja zote.
Kwa namna ya pekee mtaguso wa pili wa Vatikano tangu uitishwe ulijulikana kuwa wa kichungaji, yaani usio na lengo la kufundisha dogma mpya wala kulaani mafundisho mengine.
Msingi wa imani kuhusu mtaguso mkuu
[
hariri
|
hariri chanzo
]
Kadiri ya imani ya
Kanisa Katoliki
,
Yesu
aliwakabidhi
Mitume
kumi na wawili uongozi wa
Kanisa
wakiwa kundi moja lenye mkuu wake, yaani
Mtume Petro
.
Vilevile waandamizi wao, yaani maaskofu wote, ni kundi moja na
Papa
wa
Roma
ndiye mkuu wao. Huyo peke yake, na kundi la maaskofu likiwa pamoja naye na chini yake, ndio wenye
mamlaka
ya juu katika Kanisa lote.
Mamlaka hiyo inatumika kwa namna ya pekee unapofanyika mtaguso mkuu, yaani mkutano maalumu wa maaskofu uliokubaliwa na Papa kuwa unawakilisha kundi hilo lote.
Kwa kiasi fulani ndiyo imani ya
Waorthodoksi
pia, ingawa hao wanapunguza umuhimu wa mchango wa mamlaka ya Papa.