Mfululizo wa kurasa juu ya Yesu
|
|
|
|
Mtume Andrea
alikuwa
Myahudi
wa
karne ya 1
, mmoja kati ya wawili wa kwanza kati ya
Mitume wa Yesu
.
Anaheshimiwa na
Wakristo
wote kama
mtakatifu
, hasa
tarehe
30 Novemba
iliyo
sikukuu
yake
[1]
.
Ni
msimamizi
wa
Uskoti
,
Russia
,
Ugiriki
,
Romania
,
Malta
,
Prussia
, na wa
mabaharia
,
wavuvi
, na
waimbaji
.
Inakadiriwa alizaliwa
mwaka
6 K.K.
huko
Bethsaida
akauawa
60
hivi huko
Patrasso
(
Ugiriki
).
Jina
lake
asili
la
Kiyahudi
halijulikani. Kwa
Kigiriki
aliitwa
Ανδρ?α?
(Andreas, maana yake
Mwanamume
, Rijali). Anaitwa pia
Protocletos
yaani
Wa kwanza kuitwa
(na
Yesu Kristo
).
Agano Jipya
linasema Andrea alikuwa
ndugu
wa
Mtume Petro
,
mwana
wa Yona au Yohana (
Math
16:17;
Yoh
1:42).
Wote wawili walihamia
Kafarnaumu
ili kufanya
kazi
ya
uvuvi
, na ndipo walipoitwa na Yesu kuwa "wavuvi wa watu" (?λιε?? ?νθρ?πων,
halieis anthropon
).
Injili ya Yohane
inaarifu kuwa Andrea aliwahi kuwa
mwanafunzi
wa
Yohane Mbatizaji
, mpaka
nabii
huyo alipomuelekeza amfuate
Yesu Kristo
, "
Mwanakondoo wa Mungu
" atakayekamilisha kazi yake mwenyewe (Yoh 1:35-40). Andrea akiwa wa kwanza kumtambua Yesu kuwa
Masiya
, alimtambulisha kwa ndugu yake (Yoh 1:41).
Ni baada ya hapo kwamba waliitwa kuacha yote wamfuate Yesu (
Mk
1:17-18; Math 4:19-20;
Lk
5:11).
Katika
Injili
Andrea anatajwa mara kadhaa kuwa karibu sana na Yesu (Mk 13:3; Yoh 6:8, 12:22), lakini katika
Matendo ya Mitume
anatajwa mara moja tu, katika orodha ya
Mitume
(1:13).
Mwanahistoria
Eusebius wa Kaisarea
anataja
Asia Ndogo
,
Scizia
,
pwani
ya
Bahari Nyeusi
na
mto
Volga
hadi
Kiev
kuwa mahali pa
utume
wake baada ya
ufufuko
wa Yesu.
Mapokeo
yanadai alisulubiwa huko
Patrasso
juu ya
msalaba
wenye
umbo
la X uliopewa jina lake.
Kati ya
vitabu
vilivyokataliwa na
Kanisa
(
Decretum Gelasianum
ya
Papa Gelasio I
) kuna
Injili ya Andrea
na
Matendo ya Andrea
vilivyoandikwa
karne ya 3
.
-
Ndugu Limbourg
,
Kifodini cha Mt. Andrea
, toka Les Tres Riches Heures du duc de Berry,
Chantilly
, Musee Conde
-
-
Jose de Ribera
,
Kifodini cha Mt. Andrea
, 1628,
Budapest
, Szepmuveszeti Muzeum.
-
Kifodini cha Mt. Andrea
, karne XII,
Presencio
.
- Thenashara, Mitume Kumi na Wawili ? tafsiri ya P. A. Bunju ? Toleo la pili ? ed. Benedictine Publications Ndanda Peramiho ? Ndanda 1984 ?
ISBN 9976-63-030-1
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
|
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Mtume Andrea
kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|