Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Msaada wa Wakristo
(kwa
Kilatini
:
Auxilium Christianorum
) ni sifa mojawapo ya
Bikira Maria
katika
Kanisa Katoliki
.
Yohane Krisostomo
alikuwa wa kwanza kutumia
jina
hilo
mwaka
345
.
Baadaye,
Ukristo
ulipoatharishwa na uenezi wa
Waislamu
, waumini walimkimbilia Maria kwa jina hilo ili kupata msaada wa
sala
zake. Hasa mwaka
1571
,
Waturuki
walipokaribia kuteka
Ulaya
,
Papa Pius V
aliombea
jeshi
la Kikristo kwa kuagiza sala ya
Rozari
hadi
ushindi
ulipopatikana katika
mapigano ya Lepanto
.
Yohane Bosco
ndiye aliyeeneza zaidi
heshima
hiyo.
Mtaguso wa pili wa Vatikano
, katika
hati juu ya
Kanisa
(61, 62), ulitaja jina hilo ukieleza
umama
wa Maria
[1]
.
Sikukuu
yake huadhimishwa
tarehe
24 Mei
.
- ↑
In an utterly singular way she co-operated by her obedience, faith, hope and burning charity in the Saviour's work of restoring supernatural life to souls. For this reason she is a mother to us in the order of grace…By her maternal charity, Mary cares for the brethren of her Son who still wander through this world in the midst of dangers and difficulties until they are led to the happiness of their heavenly home".
Daniel, Michael. "Our Lady Help of Christians"
Wikimedia Commons ina media kuhusu: