Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mjomba
ni
jina
ambalo
mtoto
(wa kiume au
wa kike
) anamuita
mwanamume
ambaye ni
ndugu
(mkubwa au mdogo kwa
umri
) wa
mama
yake. Upande wa pili, mjomba anamuita mtoto huyo "
mpwa
".
Ukilinganisha na
lugha
za
Ulaya
, zile
za Kibantu
zinazingatia zaidi umri na hasa
jinsia
za
wazazi
na
ndugu
zao. Hivyo, kwa
Kiingereza
"nephew" linaweza kumaanisha "mpwa" lakini pia "mtoto" (ikiwa anayesema ni wa jinsia ileile ya mzazi).
Hivyo, anayeitwa kwa
Kiingereza
"uncle" anaweza akaitwa kwa
Kiswahili
"mjomba", lakini "baba mkubwa" (kama ni
kaka
wa
baba
) au "baba mdogo" (kama ni mdogo wa baba). Vilevile neno "aunt" linaweza kumaanisha "
shangazi
" (dada wa baba), "mama mkubwa" (kama ni mkubwa wa mama) au "mama mdogo" (kama ni mdogo wa mama).
Tena kwa
Kiingereza
"nephew" linaweza kumaanisha "mpwa" lakini pia "mtoto" (ikiwa anayesema ni wa jinsia ileile ya mzazi).
Wajibu
na
haki
kati ya mjomba na mpwa wake vinategemea
utamaduni
wa mahali. Katika baadhi ya
makabila
, kama yale yanayotia maanani
ukoo
wa
mama
kuliko ule wa baba ("
mfumojike
" au "mfumomama"), mjomba ni muhimu kuliko baba mzazi.
Pengine kwa
heshima
mtu anaweza akamuita mwingine "mjomba" ingawa hawana undugu wowote wa karibu.
Mke
wa mjomba anaitwa "mkazamjomba", au "mkazahau". Kwa lugha ya baadhi ya makabila, na zaidi mjini
Zanzibar
anaitwa "mkwe" kwa sababu watoto wake unaweza kuoana nao.
Kwa baadhi ya makabila (Mf: Wabembe) mke wa mjomba anaitwa vilevile "mjomba" au "mjomba mwanamke". Hii ni kwa kuonesha tofauti kati ya
shangazi
(yaani dada yake baba) na mjomba (kaka yake mama). Wakati huohuo kwa upande wa shangazi, ikiwa ameolewa, mume wake huitwa "babu".
|
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Mjomba
kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|