Mti
ni
mmea
mkubwa wa kudumu wenye
shina
la
ubao
.
Miti huishi miaka mingi; miti yenye
umri
mkubwa imejulikana kuwepo kwa miaka 4,800 huko
Kalifornia
. Kuna
dalili
za mti mmoja uliopimwa huko
Uswidi
kuwa na miaka zaidi ya 9,000.
Kwa jumla
ugumu
wa ubao na
uzito
wake hutegemea namna ya kukua kwa mti. Miti inayokua polepole huwa na ubao mgumu na mzito zaidi; miti inayokua harakaharaka huwa na ubao mwepesi na laini.
Ufafanuzi wa mti
Ufafanuzi wa kimataifa ni hivi:
"mti ni mmea wa ubao, kwa kawaida wenye shina
moja
tu, unakua hadi
kimo
cha angalau
mita
mbili
. Kama kuna mashina mengi, moja lifikie
unene
wa
sentimita
tano kwa kina cha kifuani cha mtu".
[1]
Muundo wa miti
Kwa kawaida mti huwa na
Shina
Unene na urefu wa shina unatofautisha mti na mimea mingine kama
vichaka
ambavyo vina shina ya ubao pia. Shina linainua majani ya mti kufikia kimo cha juu ya mimea mingine penye nuru ambayo ni chanzo cha lishe ya mti kwa njia ya
usanisinuru
. Ndani ya shina kuna seli zinazofanya kazi ya bomba na kufikisha maji hadi kilele cha matawi. Katikati ya shina ubao unakufa ni kama mfupa wa shina na kuongeza uimara wake. Gnada la nje huwa na seli zinazoendelea kujigawa na kuongeza unene.
Mti ukikatwa shina huonyesha mara nyingi duara au miviringo ambazo ni alama ya hatua za ukuaji wa mti. Kuonekana kwa duara hizi kunategemea mazingira ya mti; nje ya kanda ya tropiki kuna majira yanayosababisha vipindi vya kukua na vipindi vya kukaa kwa mti na hivyo duara mpya inajitokeza kila mwaka. Kwa hiyo mti wa aina hii unaruhusu kuona umri wake kwa kuhesabu tu idadi ya duara za shingoni.
Mizizi
Shina refu na zito linahitaji mizizi inayolingana. Mizizi huwa hasa na kazi mbili:
- inakusanya maji na lishe kwenye udongo na kuyapeleka shingoni
- ni mguu ya mti na kuushika kwenye ardhi
Miti inakuza mzizi kulingana na tabia za udongo. Penye udongo laini sana kama mchanga mti unahitaji mizizi pana inayoshikana udongo katika mazingira yake. Miti mingine inakuza hasa mzizi kama boriti.
Matawi
Matawi ni alama ya mti lakini kuna pia aina kadhaa zisizo na matawi; kwa mfano familia ya
Arecaceae
yenye miti kama
mnazi
,
mchikichi
au
mtende
hukuza majani makubwa moja kwa moja kutoka shina.
Majani
Majani yana kazi muhimu kwa mti si mapambo tu. Kuna hasa shughuli mbili
- usanisinuru
yaani kutumia nguvu ya nuru ya jua kwa kujenga
molekuli
za
glukosi
(aina za
sukari
) kama lisha yake. Kwa mazingira yake mti unasafisha hewa kwa njia hii na kutoka oksijeni.
- ugemkaji
yaani majani hugemka maji; kwa njia hii inawezesha usafiraji wa maji na lishe ndani ya mti.
Miti na ekolojia
Mwaka
2017
idadi
ya
spishi
za miti zilizojulikana ilikuwa 60,065. Karibu
nusu
ya spishi hizo ni sehemu ya
familia 10 za kibiolojia
na
asilimia
58 za spishi zinapatikana katika nchi moja tu
[2]
.
Miti ni muhimu sana kwa
ekolojia
ya
dunia
kwa sababu
- miti hushika ardhi hasa milimani kwa mizizi yake. Hivyo inazuia
mmomonyoko
wa
udongo
.
- miti hutunza kiasi kikubwa cha
maji
na kwa njia hii
hali ya hewa
duniani; miti inapokea maji ya
mvua
na kuiacha polepole.
- miti inatunza ndani yake kiwango kikubwa cha hewa ya
CO2
na kuiondoa
hewani
wakati wa kukua.
Tanbihi
- ↑
Ufafanuzi rasmi wa IUCN (International Union for Conservation of Nature and Natural Resources), kundi la Global Tree Specialist Group (GTSG) unasema: "a woody plant with usually a single stem growing to a height of at least two metres, or if multi-stemmed, then at least one vertical stem five centimetres in diameter at breast height."
- ↑
Linganisha Beech, Rivers, Oldfield, Smith: GlobalTreeSearch, angalia marejeo
Marejeo
|
Makala hii kuhusu mambo ya
biolojia
bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Mti
kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|