Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Milima ya Lebanoni
ni
safu ya milima
katika nchi ya
Lebanoni
inayoanza katika
Syria
. Inaelekea sambamba na
pwani
ya
Mediteranea
na
milima ya Lebanoni ndogo
. Mwelekeo wa safu ni kutoka
kaskazini
kwenda
kusini
kwa
urefu
wa
kilomita
240. Kati yake, kilomita 160 ziko ndani ya Lebanoni na kilomita 80 ndani ya Syria.
Upande wa
magharibi
kuna
tambarare
nyembamba kando ya pwani ya
bahari
na upande wa
mashariki
ni
bonde la Beka'a
na ng'ambo yake ni safu ya Lebanoni ndogo.
Sehemu ya juu ni
mlima
Qurnat as Sawda'
wenye
kimo
cha
mita
3,088
juu ya UB
. Kuanzia
mwezi
Novemba
hadi
Aprili
milima ya juu hufunikwa na
theluji
iliyosababisha milima kuitwa "leban" yaani
nyeupe
.
Zamani palikuwa na
misitu
minene lakini miti imekatwa tangu
nyakati za kale
na leo hii ni miti michache iliyobaki. Taarifa nyingi za
Biblia
zinataja miti ya Lebanoni iliyotumiwa kwa ajili ya
ujenzi
wa
nyumba
,
hekalu la Yerusalemu
na pia kwa
meli
(kwa mfano
Kitabu cha kwanza cha Wafalme
5:20 au
Ezekieli
27:5).
Mti
maarufu zaidi wa Lebanoni ni
mwerezi
.
Milima ilikuwa kimbilio la vikundi vingi vilivyoteswa penginepo, kwa mfano
Wakristo
Wamaroni
,
Waislamu
Washia
na
Wadruzi
.
|
Makala hii kuhusu maeneo ya
Asia
bado ni
mbegu
.
Je unajua kitu kuhusu
Milima ya Lebanoni
kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|