Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Methodio
|
Ndugu Sirili na Methodi mitume wa Waslavoni.
|
Amezaliwa
|
826
|
Feast
|
|
Methodio wa Thesalonike
(kwa
Kigiriki
: Μεθ?διο? - Methodios; kwa
Kislavoni
: Мефодии;
Thesalonike
,
Ugiriki
, mnamo
826
-
Velehrad
,
Moravia
, leo nchini
Ucheki
,
6 Aprili
885
) alikuwa
mmisionari
wa
Waslavoni
wa
Ulaya
ya
kusini
-
mashariki
katika
karne ya 9
BK
akishirikiana na
kaka
yake
Sirili
.
Tangu kale anaheshimiwa na
Wakatoliki
na
Waorthodoksi
kama
mtakatifu
pamoja na kaka yake.
Sikukuu
yao huadhimishwa
tarehe
ya
kifo
cha kaka yake,
14 Februari
[1]
.
Alizaliwa kwa
jina
la "Mikaeli"
mjini
Thesalonike
au Saloniki katika
Ugiriki
ya
kaskazini
wakati wa enzi za
Dola la Bizanti
kama
mtoto
wa Leontios
askari
wa Kibizanti na Maria
mke
wake Mslavoni.
Methodio alijiunga na
wamonaki
akawa
msimamizi
wa
monasteri
.
Mnamo
mwaka
861
Rastislav mtawala wa Moravia alitafuta njia ya kuimarisha
utawala
wake kwa kupunguza athira ya majirani wake
Wafrankoni wa Mashariki
(au
Wajerumani
jinsi walivyoitwa baadaye). Wajerumani waliwahi kuleta
imani
ya
Kikristo
Moravia. Ratislav alitaka kuwa na
maaskofu
na
mapadri
wasio Wajerumani. Hivyo alimwomba
Kaisari
wa
Bizanti
kutuma wamisionari kwake kutoka huko.
Kaisari
Michael III Konstantino
wa
Konstantinopoli
alituma ndugu Kyrilo na Methodio kwa sababu wote wawili walikuwa watu wa
Kanisa
wenye
elimu
nzuri wakijua
lugha
ya
Kislavoni
tangu
utoto
wao.
Baadaya ya kifo cha Kyrilo, Methodio aliendelea akiwa amefanywa na Papa Adriani II kuwa askofu wa
Srijem
(leo nchini
Kroatia
) na
mwalimu
wa Kikristo mwenye athira kubwa kati ya Waslavoni. Tangu mwaka
883
alitafsiri
Biblia
katika lugha ya
Kisalvoni
na kuweka misingi ya
liturgia
ya Kislavoni.
Anasifiwa kama mmisionari aliyefaulu kuunganisha ujumbe wa
Ukristo
na
utamaduni
wa Waslavoni, akifanya kazi bila kujibakiza na kwa kuvumilia vipingamizi vingi, akitegemezwa daima na Mapapa wa Roma.
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
|
Makala hii bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuiongezea habari
.
|