Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ukoo
ni
chanzo
na muunganiko wa
familia
kadhaa zenye asili moja
[1]
.
Mara nyingi huwa na
utamaduni
na
lugha
moja. Ukoo huundwa na
vizazi
mbalimbali ambapo
mila
na
desturi
zao huendelezwa na kuhifadhiwa kwa faida ya vizazi vya baadae. Mfano mmojawapo ni ukoo wa
Mkwawa
uitwao ukoo wa Mwamuyinga
[2]
.
Katika eneo la
Maziwa Makuu ya Afrika
, ukoo ni kitengo cha shirika la kijamii. Ni muundo wa zamani sana wa jamii katika eneo hilo, zaidi ya familia na kizazi. Muundo huo unapatikana katika
Rwanda
ya sasa,
Burundi
,
Tanzania
na
Uganda
.
Watu wa eneo hilo hutumia maneno tofautitofauti ya kiasili kuelezea dhana hiyo: ubwoko nchini Rwanda, umuryango nchini Burundi, ruganda katika falme za Bunyoro na Buhaya, igise huko Buha, ishanja huko Buhavu na ebika huko Buganda.
Uanachama wa ukoo ni dhana huru, yenye uwiano na
nasaba
, iliyojikita zaidi katika
utamaduni
na
imani
binafsi kuliko ushahidi halisi.
|
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Ukoo
kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|