Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mavazi
(kutoka
kitenzi
"kuvaa") ni
nguo
ambazo huvaliwa na
watu
ili kufunika
mwili
au sehemu zake. Mavazi huwa na makusudi mbalimbali:
- hukinga mwili dhidi ya
baridi
au
jua
kali pamoja na athira nyingine za mazingira zinazoweza kuathiri vibaya mwili uchi.
- huwasilisha
ujumbe
kwa watu wengine kwa kuonyesha mtu fulani ni sehemu ya kundi (k.m.
jeshi
,
timu
,
dini
,
kabila
) au
tabaka
(nguo ghali za
tajiri
) au anapendelea jambo (nembo kwenye nguo).
Kimsingi nguo zinalingana na
hali ya hewa
na
mazingira
. Penye
joto
mavazi huwa mepesi na penye baridi huwa mazito zaidi. Kila
utamaduni
umebuni aina zake za mavazi.
Historia
inaonyesha pia ya kwamba tangu kale tamaduni mbalimbali zimepokea mavazi kutoka nje na kubadilisha
mitindo
yao. Hata kama katika
majira
ya
utandawazi
watu wanavaa nguo zilezile bado wanaweza kuzitumia tofauti.
Kuna mavazi ya aina nyingi, kwa mfano ya
kitambaa
,
nguo
,
sufi
,
ngozi
au
plastiki
.
Vilevile mavazi hutofautishwa kama ni ya
wanaume
,
wanawake
au
watoto
, kama ni mavazi ya
kikazi
au ya
nyumbani
au ya
sikukuu
.
Tofauti nyingine ni kama mavazi ya chini au ya juu, au kama ni mavazi ya sehemu mbalimbali za mwili kama vile
suruali
,
mashati
,
koti
au
viatu
.
Utengenezaji
na
uuzaji
ya mavazi ni sehemu muhimu ya
biashara
na kuna kazi nyingi zinazotegemea mavazi.
Mavazi pia ni tasnia kubwa duniani inayohusisha ubunifu, uzalishaji, na mauzo ya nguo. Watu wanaweza kuchagua mavazi yao kulingana na mahitaji yao binafsi, muktadha wa kijamii, na mwenendo wa wakati huo.
|
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Mavazi
kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|