Sista

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Masista )
Masista katika maandamano wakivaa kanzu .

Sista (kutoka Kiingereza sister , yaani dada) ni neno la mkopo linalotumika katika lugha ya Kiswahili hasa kumaanisha mtawa wa kike, yaani mwanamke aliyewekwa wakfu alipoahidi kushika mashauri ya Kiinjili ya useja mtakatifu , ufukara na utiifu .