Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mapendo ya kiuchumba
ni aina mojawapo ya ma
pendo
kati ya
binadamu
.
Katika maana yake halisi, aina hiyo ni ya
maandalizi
kwa ajili ya
ndoa
.
Hapo zamani mara nyingine hakuwepo na
mapenzi
kwanza, kwani
mvulana
na
msichana
walifikia kuoana bila kuwepo kwanza
uchumba
.
Lakini kwa sasa, kutokana na
maendeleo
na
akili
kupanuka zaidi, kwa kawaida hakuna anayeoa au anayekubali kuolewa bila kumfahamu
mchumba
wake kwanza.
Ule
muda
wa kuzoeana, ndio wa mapendo ya kiuchumba, kwani haitoshi, k.mf. kumtamkia tu
mpenzi
wako kwamba ungependa awe
mama
watoto wako bila ya kuzijua
silika
,
tabia
,
hisia
zake na kadhalika. Ni vilevile upande wa pili.
Muda wa kuchumbiana ndio muda ambao wote wawili wanatakiwa kuwa makini sana, kila mmoja amsome mwenzie na kujirekebisha ili kuwezesha ndoa kudumu hata itakapojaribiwa na
maisha
.
Bahati mbaya, mara nyingi vijana hawapati
malezi
au msaada wowote wa kufaa upande huo. Sehemu nyingi wanaelekezwa tu namna ya kupunguza
hatari
ya kuambukizwa
maradhi ya zinaa
au kupata
mimba
isiyotarajiwa, kama kwamba
ngono
inawafaa katika hatua hiyo au haiepukiki kabisa.