Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Makala hii imehaririwa na
mtumiaji:Nyabsino
kwa kubadilisha lugha mara kadhaa. Nina wasiwasi kuhusu maneno mbalimbali aliyoleta. Naomba atoe ufafanuzi kuhusu maneno aliyobadilisha. Hii ni hasa maneno kama fasikebu, fasi, wafalki, mwanafasi, fataki.
Sipendi kukamtisha tamaa mwanawikipedia mpya kwa kurudisha mabadiliko haya moja kwa moja lakini nina wasiwasi kama maneno aliyetumia ni kweli lugha fasaha kwa mambo yanayojadiliwa. Kamusi zote ninazoona kama vile
KKS
,
KMM
na hasa
KAST
hazijui maneno aliyoleta kinyume zinaonyesha maneno aliyobadilisha sasa.
Naomba ataje vyanzo vyake. Halafu alirejea "taaluma ya Falaki". Naomba aangalie marejeo katika makala
astronomia
yanayotaja sababu ya kutotumia tena neno "falaki" kwa fani hii.
tunaomba pia aangalie uwepo wa neno "Explorer 1"
Kwa sasa nimelinda makala hii pamoja na
mwanaanga
Kipala
(
majadiliano
)
09:04, 4 Septemba 2014 (UTC)
[
jibu
]