Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Louis XIV
(
5 Septemba
1638
-
1 Septemba
1715
) alikuwa mfalme wa
Ufaransa
tangu
14 Mei
1643
hadi kifo chake.
Alikuwa mfalme kwa umri wa miaka minne akakabidhiwa madaraka alipotimiza miaka 21.
Louis alilenga kuunganisha mamlaka yote mkononi mwake. Alisimamia shughuli za serikali na mawaziri wote walitakiwa kutoa ripoti moja kwa moja kwake. Alitumia mapato yote ya taifa kama mapato yake mwenyewe akiamua peke yake. Alivunja upinzani wa waungwana na kuimarisha utawala wa serikali kuu katika milki yake. Alijenga uchumi wa nchi na kuendesha siasa ya nje iliyofanya Ufaransa kuwa taifa kiongozi katika Ulaya.
Katika siasa ya ndani alimaliza
Sheria ya Nantes
ulioruhusu uhuru wa kidini akapiga
Uprotestanti
marufuku na kudai watu wote wasali katika kanisa katoliki. Waprotestanti Wafaransa 200,000 waliondoka katika nchi wakikimbia
Ujerumani
hasa
Prussia
na
Uingereza
.
Alitumia pesa nyingi kwa ujenzi ya majumba ya kifalme hasa jumba kubwa la
Versailles
. Alianzisha pia taasisi za sayansi na sanaa. Utamaduni wa Ufaransa ulikuwa kielelezo kwa nchi za Ulaya.
Katika vita zake alipanusha milki yake kwa kutwaa maeneo yaliyokuwa chini ya
Hispania
,
Ujerumani
na
Uholanzi
.
Aliacha urithi wa muundo wa utawala ambako mfalme alikuwa sawa na dola na serikali.
|
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Louis XIV wa Ufaransa
kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|