Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kisiwa cha Wake
ni
atoli
(aina ya
kisiwa
) katika
Bahari ya Pasifiki
, karibu na
funguvisiwa
la
Hawaii
. Inasimamiwa na
Jeshi
la
Marekani
. Ni
eneo la ng'ambo la Marekani
, ikihesabiwa kati ya Visiwa Vidogo vya Nje vya Marekani.
Kuanzia Desemba
1941
hadi Agosti
1945
atoli hiyo ilivamiwa na
Milki
ya
Japani
.
Jinsi ilivyo na atoli nyingi,
umbo
la kisiwa ni takriban la
duara
; ukanda wa nchi kavu ni kama vipande kadhaa kwa hiyo tunaweza kusema atoli yote inafanywa na visiwa vitatu ambavyo kwa jumla huwa na eneo la
hektari
737.06.
Kisiwa cha Wake kinahesabiwa kazi ya Visiwa vilivyo mbali kabisa na
bara
au na kisiwa chochote kingine. Visiwa vilivyo karibu ni Atoli ya Bohak (
umbali
km
560, hakuna watu) na Atoli ya Utirik (km 953, kuna watu) kwenye
Visiwa vya Marshall
kwa upande wa
kusini
-
magharibi
.
Wake iko km 2,416 upande wa mashariki wa
Guam
, km 3,698 upande wa magharibi wa
Honolulu
na km 3,204 upande wa kusini-
mashariki
wa
Tokyo
.
Hakuna wakazi wa kudumu kwenye Kisiwa cha Wake, kwa hiyo hakuna
shule
ya
watoto
. Takriban watu 100 wanaishi huko wakati wowote. Wengi wao ni
wakandarasi
wanaotunza
barabara
,
uwanja wa ndege
na
miundombinu
mingine.
[1]