Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kanisa la Mt. Mikaeli
mjini
Hildesheim
(
Ujerumani
) ni mfano bora wa
usanifu majengo
wa Enzi ya kati.
Enzi ya Kati
(pia:
Zama za Kati
; kwa
Kiingereza
: "Middle Ages", pia "mediaevo" au "medievo") ni kipindi cha katikati cha
historia
ya
Ulaya
katika mgawanyo wa “zama” tatu: ustaarabu wa
ama:
Hata kama ugawaji huo umetokana na
mazingira
ya Ulaya tu, hutumiwa pia kwa maeneo mengine ya
dunia
.
Wataalamu
wengi huamini ya kwamba haufai sana kidunia lakini hadi sasa hakuna mpangilio mwingine kwa dunia yote unaoeleweka kirahisi hivi.
Kwa kawaida, Zama za Kati za Ulaya Magharibi huhesabiwa toka mwisho wa
Dola la Roma Magharibi
(
karne ya 5
) hadi kuanza kwa falme za kitaifa, mwanzo wa
uvumbuzi
wa ng’ambo ya Ulaya, kipindi cha
mwamko-sanaa
, na
Matengenezo
ya
Waprotestanti
kuanzia mwaka
1517
.
Mabadiliko hayo yalionesha mwanzo wa kipindi cha Zama za Kisasa ambacho kilitangulia
mapinduzi ya viwanda
.
Mwanzo wa kipindi cha Enzi ya Kati
[
hariri
|
hariri chanzo
]
Kabla ya Enzi ya Kati kulikuwa na
ustaarabu
wa Dola la Roma.
Milki
hiyo kubwa ilijenga
utamaduni
uliounganisha nchi za
Afrika ya Kaskazini
,
Asia ya Magharibi
na
Ulaya ya Kusini
pamoja na
Ulaya ya Magharibi
.
Katika eneo hili kubwa palikuwa na
uchumi
ulioendelea na njia za
mawasiliano
kama
barabara
,
bandari
na hata aina ya
posta
.
Ustaarabu huo ulikuwa na
idadi
ya watu waliojua kusoma na kuandika.
Lugha
za pamoja kama
Kilatini
na
Kigiriki
zilieleweka na
asilimia
fulani ya watu kote katika
dola
hili. Hata kama watu wengi, hasa watu wa
vijijini
na
watumwa
, hawakujua kusoma bado walikuwepo watu waliojua kila sehemu ya dola.
Ustaarabu huo uliporomoka pamoja na matatizo ya kiuchumi,
gharama
kubwa ya
jeshi
, kupungua kwa
uzazi
na mashambulio ya
makabila
ya nje, hasa ya
Wagermanik
, yaliyoweza kuingia ndani ya Dola la Roma bila kulingana na utamaduni wa ustaarabu huo. Roma ilishindwa kutunza utaratibu wake mbele ya mashambulio na
uhamisho mkuu wa Ulaya
.
|
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Enzi ya kati
kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|