Kanisa la Kiorthodoksi la Ethiopia
(kwa
Kiamhara
??????:??????:????:??:??????,
Yaityop'ya ortodoks tawahedo betakrestyan
) ni
madhehebu
ya
dini
ya
Ukristo
iliyotawala watu wa jamii ya
Waamhara
kwa
karne
kadhaa hadi sasa.
Wakristo hao wanaotaka kuzingatia
imani sahihi
ni sehemu muhimu katika
utamaduni
wa
Ethiopia
na
Eritrea
[1]
.
Kwa sasa ni kubwa zaidi
duniani
kuliko mengine yote ya jamii ya
Makanisa ya Kiorthodoksi ya Mashariki
, likiwa na waumini
milioni
45-50.
[2]
wengi wao wakiishi nchini Ethiopia,
[3]
lakini pia
Mashariki ya Kati
,
Ulaya
na
Amerika
.
Kanisa la Kiorthodoksi la Ethiopia linaendeleza
ushirika
na
Kanisa la Misri
tangu lilipoanzishwa na
mtakatifu
Frumensyo
aliyetumwa na mtakatifu
Atanasi
,
Patriarki
wa
Aleksandria
katikati ya
karne ya 4
BK
.
Hata hivyo mwaka
1959
lilikubaliwa liwe na Patriarki wake mwenyeji na kujiongoza.
Kwa jumla
majimbo
ni 44 na
maaskofu
60.
Kufuatana na
mapokeo
ya huko
Misri
,
Epifania
na
Pasaka
ni
sikukuu
muhimu sana, na husherehekewa kwa kufanya mambo kama vile
kufunga kula
na kucheza.
Pia kuna siku kadhaa katika
mwaka
ambapo ni
mboga
za
majani
pekee na
samaki
ndio huruhisiwa kuliwa.
Ndoa
huweza kuanzishwa au kupangwa wakati
mwanamume
ana
umri
wa miaka kumi na..., au ishirini na...
Kiutamaduni
,
wasichana
wanaruhusiwa kuolewa wakiwa na umri wa miaka 14 hadi 18, lakini katika
karne ya 20
, mambo yamebadilika, hivyo sasa umri mdogo kuliko wote wa kuolewa ni miaka 18, na suala hili linasimamiwa na
serikali
.
Ndoa za kiserikali
ni nyingi japo pia, wapo watu wanaofunga ndoa katika makani mbalimbali. Na baada ya kufunga ndoa kanisani, suala la
talaka
halipo na haliwezekani. Kila
familia
hufanya
sherehe
ya ndoa baada ya
harusi
.
Tangu kuzaliwa,
padri
hutembelea familia kwa ajili ya kumbariki
mtoto
, na pia
kutahiri
mtoto kama ni wa kiume.
Mama
wa mtoto, hutakiwa kukaa ndani kwa siku 40 baada ya kujifungua kama mtoto ni wa kiume na kukaa ndani kwa siku 80 kwa mtoto ni wa kike kabla ya kwenda kanisani kwa ajili ya
ubatizo
.
Sanaa
ya nchini Ethiopia kwa ujumla imeegamia katika masuala ya dini na michoro ya dini.
Mmoja kati ya michoro mizuri zaidi ya vitu au watu wenye
macho
makubwa na mara nyingi huwa ni watu wanaohusiana na
Biblia
.
- Archbishop Yesehaq. 1997.
The Ethiopian Tewahedo Church: an Integrally African Church.
Winston-Derek Publishers.
- Mikre-Sellassie Gebre-Amanuel. 1993. “The Bible and Its Canon in the Ethiopian Orthodox Church.”
The Bible Translator
44/1:111-123.
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
|
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Kanisa la Kiorthodoksi la Ethiopia
kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|