Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kabaka
ni
cheo
cha
mfalme
wa
Buganda
ambayo ni
ufalme
ndani ya
jamhuri
ya
Uganda
. Cheo kingine pamoja na Kabaka ni
Ssebataka
.
Tangu mwisho wa
karne ya 19
Makabaka wamekuwa
Wakristo
Wa
anglikana
wakipokea
taji
katika
kanisa kuu
la Kianglikana la
Kampala
. Makabaka wa mwisho
wamezikwa
katika
makaburi
ya
Kasubi
mjini Kampala.
Serikali
ya kwanza ya
Milton Obote
ilifuta falme zote nne za Uganda na kumlazimisha Kabaka
Mutesa II
kuondoka Uganda akipata kimbilio lake
Uingereza
.
Kati ya
1967
hadi
1993
cheo cha Kabaka hakikuwepo kisheria nchini Uganda lakini Waganda wengine walisikitikia. Serikali ya
Yoweri Museveni
ilirudisha falme za kale kama enzi za
kiutamaduni
.
Tarehe
24 Julai
1993
Ronald Muwenda Mutebi II
aliruhusiwa kurudi Uganda kutoka
Uingereza
alikokuwa amemfuata baba yake akapokea rasmi taji la Kabaka mjini Kampala.
- Kintu Kato
, mwisho wa
karne ya 14
BK
- Chwa I
, mwanzo wa
karne ya 15
- Kimera
, takriban
1420
- takriban
1447
- Ttembo
, takr. 1447 - takr.
1474
- Kiggala
, takr. 1474 - takr.
1501
- Kiyimba
, takr. 1501 - takr. 1501
- Kayima
, takr.
1528
- takr. 1528
- Nakibinge
, takr.
1555
- takr.
1582
- Mulondo
, takr. 1582- mwisho wa
karne ya 16
- Jjemba
, mwisho wa karne ya 16
- Ssuuna I
, mwanzo wa
karne ya 17
- takr.
1609
- Ssekamanya
, takr. 1609 - sehemu ya kwanza ya karne ya 17
- Kimbugwe
, sehemu ya kwanza ya karne ya 17
- Kateregga
, takr.
1636
- takr.
1663
- Mutebi I
,
Jjuuko
, na
Kayemba
takr. 1663 - takr.
1690
- Tebandeke
na
Ndawula
, takr. 1690 - takr.
1717
- Kagulu
,
Kikulwe
na
Mawanda
. takr. 1717 - takr.
1744
- Mwanga
,
Namugala
, na
Kyabaggu
, takr. 1744 - takr.
1771
- Jjunju
na
Ssemakokiro
, takr. 1771 -
1797
- Ssemakokiro
(pekee yake)
, takr. 1797 -
1814
- Kamanya
,
1814
-
1836
- Suna II
,
1836
-
1856
- Mutesa I
,
1856
-
1884
- Mwanga II
,
1884
-
1888
- Kiwewa Mutebi II
,
1888
- alijiita kabaka bila kukubaliwa na wote wakati wa Mwanga II kukaa nje
- Kalema
.
1888
-
1889
- alijiita kabaka bila kukubaliwa na wote wakati wa Mwanga II kukaa nje
- Mwanga II
(mara ya pili)
1889
-
1897
? aliporudi kutoka nje baada ya kuuawa kwa Kiweewa Mutebi na Kalema na wafuasi wake
- Daudi Cwa II
,
1897
-
1939
- Mutesa II
,
1939
-
1969
- Miaka bila Kabaka 1969 - 1993
- Muwenda Mutebi II
,
1993
? Kabaka aliyeko