Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jumuiya ya Nchi Huru
(kwa
Kirusi
:
Содружество Независимых Государств (СНГ)
,
sodrushestvo nezavisimikh gosudarstv (SNG)
; kwa
Kiingereza
:
Commonwealth of Independent States (CIS)
) ni
jina
la
umoja
wa nchi zilizokuwa sehemu za
Umoja wa Kisovyeti
hadi
mwaka
1991
.
Jumuiya hiyo iliundwa
tarehe
8 Desemba
1991 na
viongozi
wa
Urusi
,
Belarusi
na
Ukraine
.
Makao makuu
yapo
Minsk
,
mji mkuu
wa Belarusi na
wabunge
hukutana
Sankt Peterburg
.
Wanachama
- Nchi wanachama 2008 (mwaka wa kujiunga)
+ Nchi mwanachama wa kushirikishwa
+ Nchi zilizokuwa jamhuri za Umoja wa Kisovyeti zisizoshiriki katika jumuiya
Shabaha na hali ya jumuiya
Jumuiya ilianzishwa kama njia ya kuondoa Umoja wa Kisovyeti bila kuacha ushirikiano. Tangu kuundwa nchi wanachama zilitia sahihi mikataba na mapatano mengi lakini hali halisi umuhimu wa umoja huu umerudi nyuma. Marais hawakutani pamoja tangu miaka kadhaa.
Ukraine na Georgia zinaelekea kujiunga na
Ulaya
na kambi la magharibi pamoja na
NATO
na mwelekeo huo umeshasababisha ugomvi na Urusi. Moldavia vilevile inaimarisha uhusiano wake na
Romania
, ambayo ni mwanachama wa
Umoja wa Ulaya
na NATO, kwa sababu Wamoldavia wengi huongea Kiromania.
Viungo vya Nje