Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ishmaeli
(au
Ismaili
, kwa
Kiebrania
???????????, Yi?m???l: kwa
Kiarabu
????????, Ism???l) alikuwa mtoto wa kwanza wa
Abrahamu
(au Ibrahimu) na
Hagari
(au Hajiri) kadiri ya
Biblia
[1]
na ya
Kurani
.
Mungu
alikuwa amemuahidia Abrahamu uzao mkubwa kama
nyota
za mbinguni, naye akaamini ingawa alikuwa hajapata hata mtoto mmoja: ndiyo
imani
iliyompendeza sana Mungu (Mwa 15:1-6).
Lakini Abrahamu alizidi kuzeeka pamoja na
Sara
bila ya kuzaa watoto. Baada ya kusubiri muda mrefu mno Sara akamwambia azaliane na
Hagari
aliye mtumishi wa kike. Mwana huyu wa Hagar akaitwa Ishmaeli (Mwa 16:1-15). Lakini baadaye kukawa na
fitina
kati ya Sara na Hagari hivyo huyo akafukuzwa pamoja na mtoto, baada ya Sara pia akashika mimba na kumzaa mtoto
Isaka
.
Mwa 21:1-21 inatusimulia jinsi Mungu alivyotimiza ahadi yake kwa kumjalia Sara amzalie Abrahamu mtoto huyo katika uzee na utasa. Isaka ni mtoto wa imani, si wa mwili, naye ni huru, tofauti na Ishmaeli mtoto wa mtumwa ambaye hastahili kurithi pamoja na mdogo wake. Isaka, baba wa Israeli alipata baraka kuu, naye ni mfano wetu watu wa Agano Jipya. Ishmaeli alibarikiwa pia kwa ajili ya baba yake, naye ni mfano wa
Agano la Kale
ambapo watu wanategemea mambo ya kimwili (
kutahiriwa
, kunawa, kubagua vyakula n.k.) na hivyo ni watumwa (
Gal
4:21-5:1).
Kadiri ya
kitabu cha Mwanzo
alishiriki pamoja na mdogo wake
Isaka
mazishi
ya
baba
yake akafariki akiwa na umri wa miaka 137.
[2]
Ishmaeli alizaa watoto wa kiume 12 ambao wanahesabiwa mwanzo wa
Waarabu
, hasa wale wa Kaskazini.
Ishmaeli anahesabiwa
nabii
muhimu na
babu
wa
Muhammad
,
mwanzilishi
wa
dini
ya
Uislamu
.
Ingawa
Kurani
haitaji jina la mtoto ambaye Abrahamu alikuwa tayari kumchinjia Mungu, wanazuoni walifikia makubaliano kwamba alikuwa Ishmaeli, si Isaka.
- Books and journals
- Encyclopedias
- Hubert Cancik, ed. (2005).
Brill's New Pauly: Encyclopaedia of the Ancient World: Antiquity
. Brill Academic Publishers.
ISBN
978-90-04-12270-3
.
- Paul Lagasse, Lora Goldman, Archie Hobson, Susan R. Norton, ed. (2000).
The Columbia Encyclopedia
(6th ed.). Gale Group.
ISBN
978-1-59339-236-9
.
- John Bowden, ed. (2005).
Encyclopedia of Christianity
(1st ed.). Oxford University Press.
ISBN
0-19-522393-4
.
.
- Lindsay Jones, ed. (2005).
Encyclopedia of Religion
(2nd ed.). MacMillan Reference Books.
ISBN
978-0-02-865733-2
.
-
The New Encyclopædia Britannica
. Encyclopædia Britannica, Incorporated; Rev Ed edition. 2005.
ISBN
978-1-59339-236-9
.
.
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
|
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Ishmaeli
kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|