Isaac Bashevis Singer ( 14 Julai 1902 ? 24 Julai 1991 ) alikuwa mwandishi kutoka nchi ya Poland ambapo alizaliwa na jina Yitskhek Bashyevis Zinger . Mwaka wa 1935 alihamia Marekani . Hasa aliandika riwaya na insha kuhusu maisha ya Wayahudi katika karne ya 20. Aliziandika katika lugha ya Kiyiddish . Mwaka wa 1978 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi .