Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ignas wa Loyola
(kwa
Kieuskara
Inigo Loiolakoa
, kwa
Kihispania
Ignacio de Loyola
;
Loyola
,
Guipuzcoa
, leo nchini
Hispania
,
1491
-
Roma
,
Italia
,
31 Julai
1556
) alikuwa
padri
wa
Kanisa Katoliki
maarufu hasa kama
mwanzilishi
wa
Shirika la Yesu
na wa
mtindo
wa
mazoezi ya kiroho
.
Awali aliishi katika
ikulu
ya
mfalme
na katika
jeshi
, mpaka alipojeruhiwa vibaya
vitani
, ndipo alipomuongokea
Mwenyezi Mungu
. Akiwa anasoma
teolojia
huko
Paris
, alipata wenzake wa kwanza, ambao pamoja nao alianzisha
shirika
jipya huko Roma, alipofanya
utume
wenye
matunda
mengi, akiandika
vitabu
na kulea wafuasi kwa
utukufu
mkubwa zaidi wa
Mungu
.
Alitangazwa na
Papa Paulo V
kuwa
mwenye heri
tarehe
27 Julai
1609
, halafu
Papa Gregori XV
alimtangaza
mtakatifu
tarehe
12 Machi
1622
.
Sikukuu
yake huadhimishwa tarehe ya
kifo
chake
[1]
.
Pokea, Bwana, hiari yangu yote.
Pokea kumbukumbu, akili na utashi wote.
Vyovyote nilivyonavyo au kuvimiliki nimejaliwa na wewe:
nakurudishia vyote na kuukabidhi utashi wako uvitawale.
Unijalie tu upendo wako na neema yako, nami nitakuwa tajiri kutosha,
nisitamani kitu kingine chochote.
- A. JOU, S.J., Kazaliwa Kupigana Vita, Simulizi juu ya Mt. Inyasi wa Loyola kwa ajili ya Vijana (hasa wa kiume) ? tafsiri ya Ofisi ya Taifa ya Utume wa Sala, Tanzania ? ed. Ofisi ya Taifa ya Utume wa Sala, Tanzania ? Dodoma 2001 ? ISBN 0856-5589
Muhimu zaidi
Mengine
|
Makala hii bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuiongezea habari
.
|