Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Hela
ni jina kwa
pesa
lililo kawaida katika
Tanzania
. Asili ya neno ni lugha ya Kijerumani. "Heller" ilikuwa kitengo cha pesa ya
Afrika ya Mashariki ya Kijerumani
au Tanzania bara kuanzia 1904 hadi 1918. Waingereza baada ya kuchukua utawala wa koloni walibadilisha sarafu kuwa
shilingi
na
senti
lakini jina la "hela" lilibaki kwa ajili ya pesa kwa jumla.
Heller ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani
[
hariri
|
hariri chanzo
]
Tangu
1904
serikali ya
Ujerumani
ilichukua wajibu wa kutoa pesa kwa koloni yake katika Afrika ya Mashariki iliyojumlisha Tanzania bara pamoja na Rwanda na Burundi. Hadi mwaka ule
Kampuni ya Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki
iliendelea kutoa sarafu yake iliyokuwa
rupie
1 yenye pesa 64. Serikali ilipochukua jukumu hii iliamua kuendelea na rupie lakini ilibadilisha vitengo vyake vidogo kuwa Heller 100. Heller iliwahi kuwa pesa ndogo ya kihistoria katika Ujerumani lakini haikutumiwa tena tangu maungano ya Ujerumani mwaka 1871 na kuanzishwa kwa pesa ya kitaifa ya
Mark
na Pfennig.
Sarufi za Heller za Afrika ya Mashariki zilionyesha upande wa mbele neno "Heller" na namba ya thamani yake; upande wa nyumba ilikuwa na taji la Kaisari, maneno ya "Deutsch Ostafrika" (Afrika ya Mashariki ya Kijerumani) na mwaka wa kutolewa.
Heller ya Afrika ya Mashariki ilitolewa kwa sarufi za
Asili ya pesa iliyoitwa "heller" ni mji wa Kijerumani wa Hall inayoitwa leo
Schwabisch Hall
. Kule sarafu za
fedha
zilitolewa tangu mwaka
1288
zilizosambaa haraka zikaitwa "Haller" au "Heller" kutokana na jina la mji. Polepole kiasi cha fedha ndani ya sarafu kilipungukiwa hadi kuwa sarafu ya
shaba
yenye thamani ndogo.
Heller iliendelea kuwa sarafu ndogo ya kawaida (kama senti) katika Ujerumani hadi mwaka 1873 ilipofutwa baada ya kuanzishwa kwa fedha mpya ya
Mark
na
Pfennig
.
Austria-Hungaria
iliendelea kuitumia kama sarafu ndogo ya Krone hadi mwisho wa dola hili.
Chekoslovakia
kama nchi mojawapo iliyotokana na Austria-Hungaria ilikuwa nchi ya pekee kuendelea na sarafu hii kwa jina "haler". Baada ya kugawiwa kwa Chekoslovakia kuwa nchi mbili za
Ucheki
na
Slovakia
zote mbili zilkuwa na haler hadi kujiunga na
Euro
.