Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Havana
(
kihisp.
La Habana
) ni
mji mkuu
na mji mubwa wa
Kuba
kwenye 23°8
′N
82°23
′W
. Kuna wakazi milioni 2.2. Tangu
1982
mji wa kale umepokelewa katika orodha ya
urithi wa dunia
.
Mji kwa jina la Havana ulianzishwa
1515
na Mhispania
Diego Velazquez de Cuellar
lakini ulihamishwa mwaka
1519
kuja mahali pa kudumu uliopo hadi leo. Mji ukakua kuwa bandari muhimu wa kijeshi na kibiashara. Tangu 1607 Havana ilikuwa mji mkuu wa koloni ya Kihispania ya Kuba.
Havana ilikuwa hasa tangu azimio la
Hispania
la kukusanya "la flota" yaani jahazi za kubebea fedha na bidhaa za Amerika kama kundi kabla ya kuvuka
Atlantiki
kwa kusudi la kuzuia
maharamia
Waingereza waliovinda meli za Hispania. Azimio hili lilisababisha mamia ya jahazi kukusanyika katika hori ya bahari mbele ya Havana katika miezi ya Mei hadi Agosti mpaka kuanza safari ya pamoja.
Katika karne za 17 na 18 mji uliendelea kukua kuwa mji mkubwa wa tatu wa
Amerika
baada ya
Mji wa Mexiko
na Lima kushinda
Boston
na
New York
.
Mwisho wa
karne ya 19
Havana iliona mlipuko wa manowari
SS Maine
katika bandari yake tarehe
15 Februari
1898
ulioanzisha
vita ya Marekani dhidi Hispania
. Havana ilivamiwa na Waamerika na kutangazwa kuwa mji mkuu wa Jamhuri ya Kuba mwaka 1902.
Athira ya Amerika iliendelea kuwa kubwa hadi mapinduzi ya Kuba na kuingia kwa jeshi la mapinduzi chini ya
Fidel Castro
tarehe
1 Januari
1959
.