Siddh?rtha Gautama
(kwa
Kisanskrit
:
?????????
????
; kwa
Kipali
:
Siddhattha Gotama
;
563 KK
-
483 KK
) alikuwa
mwalimu wa kiroho
kutoka
India
.
Kutokana na mafundisho yake, ulianzishwa
Ubuddha
ambao unatazamwa kwa kawaida kuwa
dini
.
[1]
Katika
mapokeo
mengi ya Kibuddha anatazamwa kama
Buddha
mkuu (P.
samm?sambuddha
, S.
samyaksa?buddha
) wa wakati wetu, ambapo "Buddha" maana yake ni "aliyeamshwa" au "aliyeangazwa."
[2]
Miaka yake ya kuishi haina hakika: wanahistoria wengi wa mwanzo wa
karne ya 20
walitaja miaka
563 KK
hadi
483 KK
hivi,
[3]
lakini maoni ya siku hizi yanataja mwaka wa kufariki kati ya
486 KK
na 483 KK au, hata kati ya
411 KK
na
400 KK
.
[4]
[5]
Kadiri ya
akiolojia
, Buddha aliweza kuzaliwa huko
Lumbini
, (leo nchini
Nepal
)
[6]
[7]
[6]
au huko
Kapilavastu
,
Piprahwa
,
Uttar Pradesh
,
India
au tena
Kapileswara
,
Orissa
,
India
.
[8]
[9]
[10]
[11]
[12]
Baadaye alifundisha huko na huko India mashariki, kama vile
Magadha
na
Ko?ala
.
[13]
[14]
Gautama, anayejulikana pia kama
??kyamuni
("Mwenye hekima wa
??kyas
"), ni mwalimu mkuu wa Ubuddha, lakini anaheshimiwa pia katika dini ya
Ubanyani
, katika tapo la
Kiislamu
la
Ahmadiyya
[15]
na katika
imani
ya
Baha'i
.
Yeye alizaliwa na kupewa jina la Siddharta kutoka kwenye
familia
ya kifalme ya
ukoo
wa Shakyamuni yapata miaka 2500 iliyopita huko
India
ya kaskazini.
Mama
wa Buddha alifariki angali yeye ni mtoto na tena alikuwa na shauku la kuwa mtoto atayemzaa si wa kawaida. Akiwa
mjamzito
, aliota
ndoto
ya
Tembo
mweupe aliyehusunika na mtoto atakayejifungua.
Jambo hilo lilikuwa
dalili
ya kuonyesha kwamba mtoto atakayezaliwa atakuwa mtu mwenye
bahati
na tena maalum.
Mwona aliyetembelea jumba la kifalme ili kutoa
utabiri
wake kuhusu maajaliwa ya mtoto, kwa mujibu wa
desturi
na
mila
za siku zile, alitabiri kwamba mtoto huyo atakuja kuwa mkubwa na
mtawala
mahiri; ama ataiacha
kasri
ya
baba
yake na kuishi maisha ya kipweke kutafuta shauri kuu kuhusu Maisha na Uhai.
Babake Siddharta aliyekuwa mtawala, alishitushwa mno na kauli ya mtoto wake kuja kuwa
Mmistiya
. Hivyo alijitahidi kila aliloweza kumficha mtoto kuhusu upande wa maisha wenye sura ya
tabu
na ma
hangaiko
. Akijaribu kumsogezea na kumpa kila
fahari
ya maisha ili asahau sehemu ya
nafsi
yake yenye uwezekano wa kumfanya aghairi maisha ya
anasa
ili kwenda kuishi kimaskini kama wamistiya wengi wa zama zile walivyokuwa wakifanya, kutoka mijini na kwenda porini kuishi maisha duni na hali ya asili.
Alipofikia umri wa kuoa, baba yake alimpa
mke
ambaye alimzalia
mjukuu
mmoja. Hapo Siddharta alikuwa anatimiza miaka takribani ishirini na tisa.
Safari nne za Siddharta nje ya jumba la kifalme
[
hariri
|
hariri chanzo
]
Wakati ule Siddharta alitoka nje ya jumba la kifalme la babake kwa mara ya kwanza akiongozana na mtumishi wake mmoja mwadilifu.
Alishangaa sana alipomwona
mtu
aliyetembea kwa
shida
tu na
uso
ulikuwa na mafinyo tu. Akamwuliza mtumishi wake, "Kwa nini mtu huyu anatembea kwa shida na uso wake unaonyesha mafinyo?" Mtumishi akamjibu, "Huyu ni
mzee
. Watu wote watakuwa wazee siku mmoja. Ni hali ya kawaida". Siddharta asiyewahi kumwona mzee kwa sababu babake hakuruhusu wazee katika
mazingira
ya mtoto wake akashtuka akauliza: "Je, na mimi nitakuwa mzee na nitaonekana hivyo?". Mtumishi akamjibu, "Ndiyo, na wewe utazeeka kama kila mtu." Wakarudi kwao
kimya
.
Wakaendelea kutoka nje tena.
Safari
ya pili wakamwona
mgonjwa
, na safari ya tatu wakaona
maiti
. Kila safari Siddharta alisikia ya kwamba hata yeye mwenyewe ataona mambo haya maishani mwake. Yote yalimgusa sana akawa na
wasiwasi
kwa sababu pande hizo za maisha ziliwahi kufichwa mbele yake.
Katika safari ya nne walimwona
mtawa
wa
kihindu
aliyeketi kando ya
barabara
. Siddharta alivutwa sana na
fikra
ya kwamba mtu huyu aliachana na
mali
na mambo yote kwa
hiari
yake na kufikia
uhuru wa roho
na hakuogopa tena
kifo
.
Hapo alikata shauri moyoni mwake kuondoka katika maisha ya kifalme na kutafuta maisha ya watawa.
Siddharta aliondoka nje ya jumba la kifalme
usiku
mmoja bila ya kumwaga mtu yeyote, akajiunga na kundi la watawa na kufuata maisha yao.
Hatimaye, akiwa na wenzake alikutana nao katika
harakati
zake kutafuta kilele cha ufahamu, walikwenda kuishi kwenye misitu ya mbali na kudumu katika
kutafakari
na Milaya.
Miaka sita ilipita, iliyojaa maisha ya kujima na kila namna ya kuusonga
mwili
ili kutafuta
taamuli
. Hatimaye Siddharta mtawa alidhoofu na mwili wake kukonda kutokana na
kufunga
kwa siku mfululizo.
Siku moja akiwa mwenye kukata tamaa, akiwa kando ya
mto
, alipita
mwanamke
aliyebeba
maziwa
. Siddharta alimwomba yule mwanamke ampatie maziwa anywe, maana alikuwa mwenye kuhitaji. Basi yule mwanamke akampatia. Baada ya kunywa na kushukuru alijisikia ni mwenye
utulivu
akajisemea moyoni kwamba baada ya hapo ataketi chini ya
mti
na hatainuka tena mpaka atapotokewa na Taamuli.
Huo ukawa mwanzo mpya uliofuatiwa na
baraka
na
neema
. Kwani ni usiku uliofuatia alitokewa na Taamuli na Ufunuo. Katika imani ya Wabuddha akabadilika kuwa "Buddha" katika usiku huu yaani mtu aliyepokea
ufunuo
na
ujuzi
.
Baada ya hapo alikaa na kutafakari mambo yote aliyoyaona na kuaangalia jinsi atakavyoweza kufundisha
njia
yenye kuleta
wongofu
. Kwani Taamuli yake ilifuatia kutambua Kweli Nne kuhusu maisha.
Kweli
ya Kwanza ni kuwa Maisha ya duniani ni
mateso
kutoka kuzaliwa hadi kufa, hata kifo si mwisho kwani maisha ni mzunguko wa majira ya kufa na kuzaliwa tena na tena.
Kweli ya Pili ni kuwa
asili
ya masumbuko yote ni
Ujinga
, yaani kutokujua namna asilia na kanuni ya mambo na hali za maisha na jinsi yanavyosonga.
Kweli ya Tatu ni kwamba shida na masumbuko hutokana na kujishikiza kwa mwanadamu na mambo ya dunia hii pasipo uelewa wa lolote linalozidi
milango ya fahamu
na budi (Sehemu ya Akili yenye kuendesha fikra kutokana na milango ya fahamu).
Kweli ya Nne ni kwamba njia ya wongofu yaani namna ya kutoka katika matatizo haya aliyoiita (Njia ya Nguzo Nane).
Ni
gurudumu
la nguzo nane ambazo humuongoza mwanadamu kuelekea kwenye Taamuli na hasa kufikia wongofu. Kufikia wongofu ni kuachana na mzunguko wa kufa na kuzaliwa unaosababishwa na matakwa yenye msingi wa Budi inayojengeka na kurudisha hali za kimaisha zenye kufanya mzunguko usiokoma wa masumbuko. Hivyo, njia hii Buddha hii iliyoitwa Dhammapada (Dhamma ni
uadilifu
na Pada ni njia) ndio pekee yenye kumkomboa mwanadamu kutoka kwenye taabu na masumbuko ya
ulimwengu
. Nayo ina nguzo nane zifuatazo.
Moja ni
Ono
sahihi.
Pili ni
Dhamira
sahihi.
Tatu ni
Kauli
sahihi
Nne ni
Jitihada
Sahihi.
Tano ni
Tendo
sahihi.
Sita ni
Isho
sahihi.
Saba ni
Umakini
sahihi.
Nane ni
Mkazo nia
sahihi.
Mkazo nia ni
dhana
ya kudumu katika kitendo cha
akili
yenye kuona pasipo kusogea ama kutangatanga juu ya jambo moja hadi lingine. Na hii ndio
kigezo
kikuu cha Siddhaharta Buddha katika kufundisha Milaya yenye kuongoza kwenye Taamuli. Pia tazama
Vipassana
.
- ↑
Boeree, George.
"An Introduction to Buddhism"
. Shippensburg University
. Iliwekwa mnamo
2011-09-10
.
- ↑
Turner, Sir Ralph Lilley
(1962?1985).
"buddha 9276"
.
A comparative dictionary of the Indo-Aryan languages. London: Oxford University Press
. Digital Dictionaries of South Asia, University of Chicago. uk. 525. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka
chanzo
mnamo 2012-07-17
. Iliwekwa mnamo
22 Februari
2010
.
Hypothetical root
budh
"perceive" 1. Pali
buddha
? "understood, enlightened",
masculine
"the
Buddha
"; A?okan (the language of the
Inscriptions of A?oka
)
Budhe
nominative
singular
;
Prakrit
buddha
? ' known, awakened ';
Waigal?
b?d??
, "truth";
Bashkar?k
budh
"he heard";
T?rw?l?
b?do
preterite
of
b?
, "to see, know" from
b?dhati
;
Phal??a
buddo
preterite of
bu??
, "to understand" from
budhyat?
;
Shina
Gilgit? dialect
budo
, "awake"; Gur?s? dialect
budy?n?
intransitive
"to wake";
Kashmiri
b??du
, "quick of understanding (especially of a child)";
Sindh?
?udho
, past
participle
(
passive
) of
?ujha?u
, "to understand" from
budhyat?
, West
Pah???
buddh?
, preterite of
buj??
, "to know";
Sinhalese
buj
(
j
written for
d
),
budu
,
bud
,
but
, "the Buddha".
- ↑
L. S. Cousins (1996), "
The dating of the historical Buddha
Archived
26 Februari 2011 at the
Wayback Machine
.: a review article",
Journal of the Royal Asiatic Society
(3)6(1)
: 57?63.
- ↑
See the consensus in the essays by leading scholars in
The Date of the Historical ??kyamuni Buddha
(2003) Edited by A. K. Narain. B. R. Publishing Corporation, New Delhi.
ISBN 81-7646-353-1
.
- ↑
"If, as is now almost universally accepted by informed Indological scholarship, a re-examination of early Buddhist historical material, ..., necessitates a redating of the Buddha's death to between 411 and 400 BCE...." ?Paul Dundas,
The Jains
, 2nd edition, (
Routledge
, 2001),
p. 24.
- ↑
6.0
6.1
"Lumbini, the Birthplace of the Lord Buddha"
. UNESCO
. Iliwekwa mnamo
26 Mei
2011
.
- ↑
"Nakala iliyohifadhiwa"
. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka
chanzo
mnamo 2012-10-31
. Iliwekwa mnamo
2011-10-29
.
- ↑
"Kapilavastu"
. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka
chanzo
mnamo 2011-01-08
. Iliwekwa mnamo
1 Machi
2011
.
- ↑
"Nakala iliyohifadhiwa"
. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka
chanzo
mnamo 2013-06-03
. Iliwekwa mnamo
2011-10-29
.
- ↑
http://www.rediff.com/news/2002/sep/16spec.htm
- ↑
http://www.srilankaguardian.org/2008/03/buddha-born-in-orissa-scholars.html
- ↑
http://orissa.gov.in/e-magazine/Journal/jounalvol1/pdf/orhj-3.pdf
- ↑
Warder, A.K.
Indian Buddhism
. 2000. p. 45
- ↑
Skilton, Andrew.
A Concise History of Buddhism.
2004. p. 41
- ↑
Islam and the Ahmadiyya jama?at
Retrieved on Februari 2011
- Ambedkar, B.R.
(1957).
The Buddha and His Dhamma
. Bombay: People's Education Society.
- Armstrong, Karen (2001).
Buddha
. New York: Penguin Books.
- Bechert, Heinz, mhr. (1996).
When Did the Buddha Live? The Controversy on the Dating of the Historical Buddha
. Delhi: Sri Satguru.
- Conze, Edward, trans. (1959).
Buddhist Scriptures
. London: Penguin Books.
{{
cite book
}}
: CS1 maint: multiple names: authors list (
link
)
- N??amoli, Bhikku (1992).
The Life of the Buddha According to the Pali Canon
(toleo la 3rd). Kandy, Sri Lanka: Buddhist Publication Society.
- Ortner, Jon (2003).
Buddha
. New York: Welcome Books.
- Rahula, Walpola (1974).
What the Buddha Taught
(toleo la 2nd). New York: Grove Press.
- Reps, Paul;
Senzaki, Nyogen
(1957).
Zen Flesh, Zen Bones: A Collection of Zen and Pre-Zen Writings
. New York: Doubleday.
- Robinson, Richard H.; Johnson, Willard L.; Wawrytko, Sandra A.; DeGraff, Geoffrey (1996).
The Buddhist Religion: A Historical Introduction
. Belmont, CA: Wadsworth Publishing Co.
- Sathe, Shriram (1987).
Dates of the Buddha
. Hyderabad: Bharatiya Itihasa Sankalana Samiti.
- Senzaki, Nyogen
; McCandless, Ruth Strout (1953).
Buddhism and Zen
. New York: Philosophical Library.
|
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Gautama Buddha
kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|