Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Fransisko wa Paola
(kwa
Kiitalia
Francesco da
Paola
;
27 Machi
1416
?
2 Aprili
1507
) alikuwa
mtawa
nchini
Italia
.
Ametambuliwa na
Kanisa Katoliki
chini ya
Papa Leo X
kuwa
mtakatifu
kuanzia
mwaka
1519
.
Tarehe ya
kifo
chake, yaani
2 Aprili
, pia ni
sikukuu
yake
[1]
.
Fransisko alizaliwa kwa
muujiza
katika
mji
wa
Paola
,
mkoa
wa
Calabria
,
Italia
, mwaka 1416.
Wazazi
wake walikuwa wamefikia
uzee
bila ya kuweza kuzaa, lakini walimuomba
Fransisko wa Asizi
na kuweka
nadhiri
kuwa
mtoto
wao ataitwa Fransisko. Ndipo walipojaliwa kuzaa.
Tangu
utotoni
alishika
maisha
magumu ya
sala
na
toba
upwekeni
.
Alianzisha
shirika la watawa
wakaapweke
, ambalo baadaye likawa
Utawa wa Wadogo Kabisa
, likapata kibali kutoka kwa
Papa
mwaka
1506
. Pamoja na kuahidi
mashauri ya Kiinjili
matatu ya kawaida, wanaahidi pia kuishi daima kwa toba kama wakati wa
Kwaresima
.
Kanuni
yake ni ya pekee, ingawa inafuata kwa jumla ile ya
Ndugu Wadogo
ikiiongezea
malipizi
makali ya
mababu wa jangwani
na katazo la kugusa
pesa
. Badala yake alitaka hao
Waminimi
waishi kwa kupokea misaada bila kumiliki chochote
Kaulimbiu
yake ilikuwa
neno
"caritas" (kwa
Kilatini
, "
upendo
").
Fransisko alifariki mwaka 1507 huko
Tours
,
Ufaransa
alipokuwa ametumwa na
Papa
kwa ombi la
mfalme
Alois XI
aliyemtaka karibu naye wakati wa kufa
[2]
.
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
|
Makala hii bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuiongezea habari
.
|