Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rais Felix Tshisekedi.
Felix Antoine Tshisekedi
(alizaliwa
13 Juni
1963
) ni
kiongozi
wa
chama
cha Muungano wa Demokrasia na Maendeleo ya Jamii (
UDPS
), chama cha zamani na chama cha upinzani cha
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
.
Mwishoni mwa mwaka
2008
, Tshisekedi alitajwa kuwa
Katibu Mkuu
wa UDPS wa mahusiano ya nje. Mnamo Novemba
2011
, alipata kiti katika
Bunge
la Taifa, akiwakilisha
mji
wa
Mbuji Mayi
katika
mkoa
wa
Kasai-Mashariki
.
Tarehe
10 Januari
2019
, ilitangazwa kwamba Tshisekedi amechaguliwa kuwa
rais
wa nchi katika uchaguzi mkuu wa tarehe
30 Desemba
2018
, kwa kuwashinda
Martin Fayulu
na
Emmanuel Ramazani Shadary
.
Baada ya Fayulu kukata
rufaa
, tarehe
19 Januari
Mahakama Kuu ilithibisha
ushindi
wa Tshisekedi, ingawa
Umoja wa Afrika
,
Kanisa Katoliki
na nchi kama
Ufaransa
wa
Ubelgiji
walipinga tena.
|
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Felix Tshisekedi
kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|