Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Eneo la utawala
ni sehemu ya
nchi
iliyotengwa kwa madhumuni ya
utawala
. Kwa kawaida kuna ngazi tofauti za
ugatuzi
kama vile
mkoa
,
wilaya
,
tarafa
,
kata
/
shehia
na
kijiji
na kila moja ina
madaraka
yake.
Madaraka ya kila ngazi ya utawala hutegemea
katiba
na
siasa
ya nchi.
- katika kila mfumo kuna uwezekano kwamba maeneo ya ngazi ya chini kama
manisipaa
,
miji
, kata au vijiji huwa na madaraka ya pekee yanayotajwa katika katiba ya nchi.
Majina ya vitengo vya kiutawala hutofautiana kati ya nchi na nchi. Kwa kusudi la kulinganisha hutajwa mara nyingi kufuatana na ngazi chini ya serikali kuu
- ngazi ya kwanza: eneo lililo moja kwa moja chini ya ngazi ya kitaifa; mfano
mikoa ya Tanzania
,
kaunti za Kenya
,
majimbo ya Marekani
- ngazi ya pili: ni vitengo chini ya eneo ngazi ya kwanza; mfano ni
wilaya
za Tanzania, sub county za Kenya. Katika nchi nyingi miji mikubwa hupangwa hapa
- ngazi ya tatu: ni migawanyo ya maeneo ya ngazi ya pili; mfano ni
tarafa
za Tanzania
- ngazi ya nne na ya tano ni migawanyo tena ya maeneo katika ngazi za juu. Mara nyingi vijiji, miji midogo au maungano ya vijiji hupangwa hapa. Mfano ni
kata
na
vijiji
au mitaa katika Tanzania.
|
Makala hii kuhusu mambo ya sheria bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Eneo la utawala
kama historia yake au uhusiano wake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|