Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Dominiko Nguyen
(
1802
-
1862
) alikuwa
tabibu
ambaye alifungwa pamoja na
wakulima
Dominiko Nhi
,
Dominiko Mao
,
Vinsenti Tuong
na
Andrea Tuong
kwa ajili ya
imani
ya
Kikristo
.
Baada ya kuteswa kwa muda mrefu
gerezani
, walikatwa
kichwa
chini ya
kaisari
Tu Duc
[1]
.
Ni mmojawapo kati ya
Wakristo
wafiadini wa Vietnam
waliouawa
kwa ajili ya
imani
yao huko Vietnam katika
karne ya 17
,
18
na
19
(
1625
?
1886
).
Wanatajwa pia kama
Watakatifu
Andrea D?ng-L?c
na wenzake 116.
Kwa nyakati tofauti,
Papa Leo XIII
,
Papa Pius X
na
Papa Pius XII
waliwatangaza kuwa
wenye heri
, halafu
Papa Yohane Paulo II
aliwaunganisha katika kuwafanya
watakatifu
wafiadini
tarehe
19 Juni
1988
.
Sikukuu
yao huadhimishwa kwa pamoja kila tarehe
24 Novemba
, lakini ya kwake mwenyewe tarehe
16 Juni
[2]
.
- ↑
https://www.santiebeati.it/dettaglio/57470
- ↑
Martyrologium Romanum
- Les Missions Etrangeres. Trois siecles et demi d'histoire et d'aventure en Asie
Editions Perrin, 2008,
ISBN 978-2-262-02571-7
- "St. Andrew Dung-Lac & Martyrs"
, by Father Robert F. McNamara, Saints Alive and All God's Children Copyright 1980-2010 Rev. Robert F. McNamara and St. Thomas the Apostle Church.
- "Vietnamese Martyr Teaches Quiet Lessons"
, By Judy Ball, An AmericanCatholic.org Web Site from the Franciscans and St. Anthony Messenger Press.
|
Makala hii bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuiongezea habari
.
|