Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Diane Kruger
|
|
Amezaliwa
|
Diane Heidkruger
15 Julai
1976
(
1976-07-15
)
(umri 47)
|
Kazi yake
|
Mwigizaji
|
Miaka ya kazi
|
2002?mpaka sasa
|
Ndoa
|
Guillaume Canet
(m. 2001?2006) (ametalikiwa)
|
Diane Kruger
(amezaliwa tar.
15 Julai
1976
) ni mwigizaji wa filamu na mwanamitindo wa zamani kutoka nchini
Ujerumani
. Huko
Amerika ya Kaskazini
, Anafahamika zaidi kwa uhusika wake wa Helen kwenye filamu ya
Troy
, Dr. Abigail Chase kwenye
National Treasure
na
National Treasure: Book of Secrets
, na Bridget von Hammersmark kwenye
Inglourious Basterds
.
Kruger alizaliwa kama
Diane Heidkruger
mjini
Algermissen
,
Ujerumani
, karibu na
Hildesheim
. Ni binti wa mwajiriwa wa benki Bi. Maria-Theresa na mtaalamu wa masuala ya kompyuta Bwana Hans-Heinrich Heidkruger.
[1]
Alilelewa katika mazingira ya dhehebu la
Kiromani Katoliki
[2]
kuhitimu elimu yake ya awali katika shule za Kikatoliki kabisa.
[3]
Diane hakuwahi kunywa pombe hadi alipofikisha umri wa miaka 20, kwa sababu aliona kasoro na athari za ulevi kupitia kwa baba'ke.
[4]
Mama yake alimsomesha Diana katika vipindi tofauti ili aongeze tija lugha ya Kiingereza kwa mwanawe. Alilelewa nchini Ujerumani akiwa na mdogo wake wa kiume, Stefan.
Akiwa msichana, Kruger alitaka hasa kuwa ballerina na kwa bahati akafanikiwa kuchaguliwa kwenye shule ya balleti ya
Royal Ballet School
ya mjini
London
. Hata hivyo, baada ya kuumia imepelekea aache kazi ya ballet ikiwa bado changa kabisa, Kruger akahamia mjini
Paris
na kubadilisha nguvu zake upande wa uanamitindo.
[5]
Wikimedia Commons ina media kuhusu: